Walimu Walezi wa Watoto wanaofundisha kwenye vituo vya kulelea watoto wadogo Day Care Centres) wakiwa katika semina ya kuwajengea uwezo iliyotolewa na Chuo cha Mafunzo ya Walimu Montessori Ushirika wa Neema Moshi.MOSHI-KILIMANJARO.
Walimu wa malezi na makuzi ya watoto, wametakiwa kuwa na lugha nzuri pindi wanapokuwa wakituo huduma kwenye vituo vyao vya kazi ili kujenga urafiki mzuri na watoto hao.
Wito huo umetolewa Septemba 13,2024 na Mkuu wa Chuo cha Mafunzo
ya Walimu Montessori Ushirika wa Neema Moshi, Christina Nakey, wakati wa semina
ya kuwajengea uwezo walezi wa watoto hao kutoka Manispaa ya Moshi na
Halmashauri ya Moshi Vijiji, wanaofundisha kwenye vituo vya kulele watoto (Day Care Centers).
Nakey amesema wako baadhi ya watoto wengi wanapitia changamoto
nyingi miongoni mwa walezi wao, wana jamii, pamoja na mazingira duni
wanamoishi, hivyo ni vizuri wakawapokea kwa upendo na kuzungumza nao kwa lugha
ya upole.
Katika semina hiyo mkuu huyo wa Chuo liweza kuwafundisha madi
inayohusu swala la saikolojia kwa walezi hao, pindi watakaporejea elimu hiyo iweze kuwasaidia kuwatambua watoto
pindi wanapokuwa wakikabiliwa na changamoto
za msongo wa mawazo.
Amesema ziko changamoto mbalimbali ambazo watoto wanapozipitia
ikiwemo kupoteza wazazi wazazi wao, ugomvi katika familia, kukosa mahitaji ya
msingi ya kimwili na kisaikolojia na masimango kwa mtoto kuna msabishia mtoto
huyo kuwa na msongo wa mawazo,
Naye Makamu Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Montessori Ushirika wa
Neema Moshi Lilian Kimaro, semina hiyo ilikuwa ya siku nne, ambapo
waliamua kuiandaa kwa ajili ya kuwajengea uwezo walezi wa watoto, namna
ambavyo wanapaswa kuwahudumia watoto wawapo kwenye vituo vyao.
“Watoto wengi wanapitia katika changamoto nyingi ikiwemo
kunyanyaswa, kupigwa na kubakwa,” amesema Mwl. Kimaro.
Akizungumza mshiriki wa semia hiyo Rehama Makule, amesema wako baadhi ya watoa huduma za malezi na makuzi wasio kuwa na taaluma ya kuwalea watoto, wakati mwingine wamekuwa wakiona kama wanawasaidia watoto hao kumbe huwaharibu zaidi.
Aidha amesema somo la saikolojia lililofundishwa na Mkuu cha chuo hicho limetusaidia wao kama walimu wa ma;lezo na makuzi ya mtoto namna ya kuwasaidia watoto hao pindi wanapokuwa na changamoto kama hiyo.
Nao baadhi ya washiriki wa semina hiyo Rajab
Shaban Kyatwa Mary Manyanga na Catherine Joshua, wameushukuru uongozi wa Chuo
cha Mafunzo ya Walimu Montessori Ushirika wa NeemaMoshi, kwa kuwaandalia semina
hiyo ambapo wamesema imetasaidia
kutambua jinsi ya kuwalea watoto, hususani wanaotoka katika mazingira magumu
ili kuweza kuwapa malezi bora ikiwa ni pamoja na kuwajenga kisaikolojia.
Akifunga semina hiyo Afisa Ustawi wa Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Moshi Habiba Bhou, amesema mafunzo kwa walezi wa watoto yatawasaidia kuboresha huduma kwa watoto wanaowahudumia kwenye vituo vyao.
Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Walimu Montessori Ushirika wa Neema Moshi, Christina Nakey, akiwafundisha semina ya kuwajengea uwezo walezi wa watoto kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Moshi na Moshi Vijijini.
Walimu wa Malezi na makuzi ya Watoto wakiwa darasani
Mshiriki wa semina ya kuwajengea uwezo Mwl. Rehema Makule, aliyevaa blauzi nyekundu akifuahia somo la Saikolojia lililokuwa likifundishwa na Mkuu wa Chuo cha Walimu Montessori Ushirika wa Neema Moshi Sr. Christine Nakey.
Mwl. Catherine Joshua wa kwanza kulia, akifuatilia kwa makini mada iliyokuwa kifundishwa na Mkuu wa Chuo cha Montessori Ushirika wa Neema Moshi.
Majengo ya Chuo cha Walimu Montessori Ushirika wa Neema Moshi










