MOSHI-KILIMANJARO
HALMASHAURI Kuu ya Chama
Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Moshi Vijijini, Mkoani Kilimanjaro, imeupongeza
uongozi wa Wakala ya Usambazaji Maji na Usafi na Mazingira Vijijini (RUWASA)
kwa kutekeleza miradi ya maji ambayo imeweza kutatua changamoto za uhaba wa
maji ambao ulikuwa ukiwakabili wananchi wengi wilayani humo.
Mwenyekiti wa CCM Moshi
Vijijini Cyril Mushi alitoa pongezi hizo Septemba 13,2024 wakati kikao cha
halmashauri hiyo kilichofanyika Ukumbi wa mikutano wa Ofisi za CCM mkoani humo.
Amesema moja ya changamoto
kubwa ambazo huwakabili wananchi ni ile ya upatikanaji wa Maji Safi na Salama; huku
akiwapongeza RUWASA Moshi Vijijini kazi kubwa ya kukabiliana na changamoto hiyo
kwa kutekeleza miradi mingi ya maji.
Akiwasilisha taarifa ya
utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025 kwenye kikao hicho kwa niaba
ya Mkuu wa Wilaya ya Moshi James Kaji, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya
ya Moshi David Mgonja, amesema moja wapo ya kazi kubwa iliyofanywa ni kuboresha
na kuimarisha miundombinu ya maji.
Amesema moja ya kazi
zilizofanyika ni pamoja na ukukarabati mradi ya maji Marangu katika kata za
Marangu Magharibi na Marangu Mashariki
ambapo mradi huo unahudumia vijiji 11, na kwamba utekelezaji wake umefikia
asilimia 70.
Amesema katika kutekeleza
miradi hiyo ya maji, wananchi katika vijiji 9 vya kata za Kibosho Kirima,
Kibosho Kati, Okaoni na Kirua Vunjo watanufaika na utekelezaji wa miradi ambayo
inaendelea kufanyika huko.
Akizungumzia ukusanyajin wa
mapato Afisa Mipango huyo amesema Halmashauri hiyo imeendelea kuimarisha
ukusanyaji wa mapato kwa kuboresha mifumo ya ukusanyaji wa mapato hayo.
Vilevile amesema katika
kipindi cha miaka minne kuanzia mwaka 2020/2021 na 2023/2024 ukusanyaji wa
mapato umeongezeka kutoka Sh bilioni 2.9 na kufikia Sh bilioni 4.1 mwaka 2023/2024.
Aidha amesema kuwa Halmashauri hiyo pia imeendelea kubuni vyanzo vipya vya mapato ikiwemo kuanzishwaji wa Standi mpya ya daladala eneo la Sango.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya
Moshi Vijijini Cyrili Mushi, akisisitiza jambo wakati akiendesha kikao cha
Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Moshi Vijijini.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi Vijijini Shadrack Mhagama (Kulia) akijadiliana jambo na Katibu wa CCM Wialaya ya Moshi Vijijini Ramadhan Mahanyu.
Mjumbe wa Baraza KUU (UVCCM)Taifa Victor Makundi, akisalimia na Katibu wa CCM Wilaya ya Moshi Vijijini Ramadhan Mahanyu, baada ya kumalizika kwa kikao cha Halmashauri KUU ya CCM Wilaya ya Moshi.
Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Makuyuni Sunday Abdul Chilembwe wa kwanza kushoto, Mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM Taifa Victor Makundi katikati na Emmanuel Mlaki wa kwanza kulia wakibadilishana mawazo mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Moshi Vijiji nje ya Ofisi za CCM Mkoa wa Kilimanjaro
Mjumbe wa Baraza KUU (UVCCM)Taifa
Victor Makundi, alisalimia na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Moshi Emmanuel Mlaki.
Wakili Msoni Emmanuel Mlaki
(Kulia) akiteta jambo na Mjumbe wa Baraza KUU (UVCCM)Taifa Victor Makundi.





