MOSHI-KILIMANJARO
Mkazi wa Jimbo la Moshi Mjini Francis Sebastian Kimario kwa jina
maarufu (Yeboyebo), amesema Mbunge wa Jimbo hilo Priscus Tarimo, hapigwi vita
na vyama vya upinzani bali wanaompiga vita ni wana CCM wenyewe.
Hayo ameyasema Septemba 12, 2024 mjini Moshi, wakati akizungumza na
KISENA BLOG, kuhusiana na fedha za miradi ya maendeleo alizozileta katika jimbo
hilo.
Kimario amesema kuwa ameridhishwa na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, huku wakimtaka Mbunge wa Jimbo hilo Priscus Tarimo asihangaike kuelezea sana miradi hiyo ya kimaendeleo kwani juhudi zake zinamtambulisha kwa kazi alizozifanya.
Kimario amesema kuwa wako baadhi ya wana
CCM wamekuwa wakimpiga vita, ili kumfifisha na juhudi zake ambazo amekuwa
akizifanya za kuwaletea maendeleo wananchi wa jimbo la Moshi Mjini.
“Vyama vya upinzani vilivyopo Moshi mjini havimpigi vita Mbunge wa
Jimbo la Moshi Mjini Priscus Tarimo, wanaompiga vita ni wana CCM wenyewe.”amesema
Kimario.
Ameongeza kluwa “Tunaishukuru sana Serikali kwa kutenga fedha zaidi ya
Sh bilioni 2 kwa ajili ya ujenzi wa jengo jipya kwa ajili ya Kitengo cha huduma
za upasuaji ndani ya Hospitali yetu ya Rufaa ya Mkoa wa Mawenzi.
Amesema kazi ya mbunge ni pamoja na kwenda kutusemea sisi wananchi ambao kwa namna moja ama nyingine hatuna fursa ya kwenda wenyewe Bungeni, tumeshuhudia fedha za maendeleo ambazo amezipigania na kuweza kuletwa kwa ajili ya shughuli za maendeleo hivyo niwaombe wananchi wenzangu wa Jimbo la Moshi Mjini tuendelee kumuunga mkono mbunge wetu Priscus Tarimo bila kujali tofauti zetu za itikadi, dini au rangi.
Akizungumza na wananchi hao Mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini Priscus Tarimo, amesema kwa kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan Serikali Jimbo la Moshi mjini imepokea zaidi ya Sh bilioni 23 fedha za miradi ya maendeleeo zilizotumika katika ujenzi wa shule mpya, vyumba vya madarasa, jengo la utawala, vituo vya afya na hospitali ya Manispaa.
“Katika kipindi hiki ambacho nimekuwepo katika nafasi hii ya Ubunge Jimbo la Moshi Mjini, tumpata fedha nyingi sana za maendeleo kuliko kipindi kingine chochote, niwahakikishie fedha nyingi za maendeleo zilizokuja katika Jimbo la Moshi mjini,”
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi Mwl. Mwajuma Nasombe, ameishukuru serikali kuu kwa kutoa fedha nyingi za za maendeleo ambazo zimetumika kwa ajilim ya shughuli za miradi mbalimbali ya maendeleo ndani ya Manispaa hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini Priscus Tarimo, akifafanua jambo wakati alipokuwa akizungumza na KISENA BLOG

