Kusanyiko la wamama wajane kata ya Korongoni Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, wakiwa katika maombi maalumu ya kumuombea Raisa Samia Suluhu Hassan
KORONGONI-MOSHI
Wanawake Wajane Kata ya
Korongoni Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, wamefanya dua fupi ya kumuombea
Rais Samia Suluhu Hassa pamoja na kuiombea nchi kuwa katika hali ya amani na
utulivu katika kipindi cha kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa na uchaguzi
mkuu mwaka 2025.
Dua hiyo ambayo
ilishirikisha viongozi wa madhebu ya dini, wazee mashuhuri, viongozi wa Chama
na Serikali ambayo ilifanyika katika shule ya Msingi Korongoni.
Akizungumza mara baada ya
kufanyika kwa dua fupi ya kuliombea Taifa Sheikhe wa Msikiti wa Riadha Thabit
Tarimo, mewataka wajane wasikate tamaa ya maisha au kujiona wanyonge pale
wanapoondokewa na wenza wao;
Huku akimshukuru Diwani wa Kata hiyo kwa upendo ambao ameuonesha kwa Wajane hao kwa kuweza kuwakutanmisha kwa pamoja na kuweza kufanya dua hiyo sambamba na kula chakula nao cha mchana.
Naye mdau wa maendeleo mkoani Kilimanjaro Alhaji Ibrahim Shayo, amesema kuna mengi yanayowakumba wajane baada ya kufiwa na waume zao, kwani wengine hupambana na kufanikiwa kusonga mbele, lakini wengine hujikutana na maisha magumu wao na hata familia zao.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Korongoni Heavenlight Kiyondo, amesema unapokuwa kiongozi mwanamke ziko changamoto nyingi ambazo anakuwa akizipitia, ikiwemo kuumizwa kwasababu tu ya kuwa kiongozi mwanamke.
Zaidi ya Wanawake Wajane 50
kutoka katika Kata ya Korongoni walishiriki dua fupi ya kumuombea Rais Samia
Suluhu Hassan pamoja na kuiombea nchi kuwa katika kuelekea ucghaguzi wa
Serikali za Mitaa na uchaguzi mkuu 2025.




