MOSHI-KILIMANJARO.
Wakuu wa vitengo vya
usimamizi wa ununuzi na ugavi, wakuu wa idara za mipango sekretarieti za mikoa
na halmashauri, wametakiwa kujikita zaidi kuzitumia takwimu pindi
wanapofanya manunuzi ya umma.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, Kiseo Yusuf, ametoa wito Septemba 18,2024 wakati akifungua Mkutano wa Kikanda, uliofanyika mkoani humo ukiwa na lengo la kuwakumbusha na kuwahimiza wataalam hao wanapofanya kazi zao kuzingatia Sheria ya ununuzi ya umma.
Nzowa amesema kuwa kutokana na fursa zilizopo katika Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sheria hiyo italeta tija endapo watu wanaohusika na masuala ya ununuzi wa Umma wataifuata sheria hiyo na taratibu zote za ununuzi wa Umma.
“Matumizi ya Takwimu yana umuhimu mkubwa sana
katika manunuzi ya umma, moja yanasaidia halmashauri zetu
ua mikoa yetu kununua vitu kulingana na mahitaji yaliyopo, unapotaka kujenga
shule katika wilaya au halmashauri flani ni lazima manunuzi yale yafanyike kulingana na mahitaji
yaliyopo kwa wakati huo, pasipo kuzidisha wala kupunguza.”amesema.
Amesema kama Wataalam
hawataweza kuzingatia takwimu wanaweza kufanya manunuzi ambayo wanaweza kuzidisha bila sababu
ama kupunguza kwa kuwa hawana takwimu sahihi.
Amesema “Tumeona
mabadiliko mazuri yaliyopo kwenye Sheria mpya ya ununuzi wa umma,
ambayo kwa kiasi kikubwa yananufaisha wazawa, wito wangu kwa wanaohusika
na manunuzi waifuate Sheria hii."
Kwa upande wake Meneja
wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi
wa Umma (PPRA) Kanda ya Kaskazini, Magai
Maregesi, amewashauri Watanzania kujisajili kwenye mfumo mpya wa Kielektroniki
wa Ununuzi wa Umma (NeST), ili kunufaika na Sheria hiyo inayotoa fursa za kiuchumi kwa wananchi wote wakiwamo
wanawake, vijana na watu wenye ulemavu
‘’Nawasihi Watanzania
kuacha kukwepa Mfumo wa NeST kwa kuwa kuna fursa nyingi kwenye Sheria ya Ununuzi ikiwemo fursa za biashara na uwekezaji, bila
kujisajili wazabuni hawatatambua uwepo wao kwa wepesi’’ Amesema Maregesi.









