Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Geophrey Pinda amekabidhi Hati Miliki za Ardhi 250 kwa wananchi wa
Tarakea wilayani Rombo Mkoani Kilimanjaro.
Pinda amekabidhi hati hizo leo Septemba 18,2024 katika hafla
fupi iliyofanyika Soko la Mbomai Wilayani Rombo Mkoani Kilimanjaro ambako
Kliniki ya Ardhi ilifanyika sanjari na kupokea kero na changamoto za migogoro
ya ardhi.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Naibu Waziri wa Ardhi Pinda
amewataka wananchi waliokabidhiwa hati kuhakikisha wanazihifadhi na kuzitunza
kwa umakini pasipo kuifungasha na vitu vigumu (Lamination).
Aidha amesema hati milki
za ardhi walizokabidhiwa wananchi wa Rombo ni nyaraka nyeti na zina faida kubwa
ikiwemo kuaminiwa kupata mikopo kutoka taasisi za kifedha nchini.
Aidha Pinda amemuelekeza Kamshina Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa
Kilimanjaro Rehema Mdee, kuendesha zoezi la kliniki ya ardhi katika wilaya hiyo
kwa siku tatu kuanzia Septemba 25 hadi 27 Mwaka huu
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Grophrey Pinda yuko katika ziara ya kikazi mkoni Kilimanjaro ambapo mbali na mambo mengine atasikiliza na kutatua changamoto za ardhi kwa wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro.

.jpg)


