MOSHI-KILIMANJARO
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Geophrey Pinda, amewataka wananchi waliokabidhiwa Hati Milki za Ardhi kuhakikisha wanazitunza ili kuepuka udanganyifu unaoweza kufanyika kutoka kwa watu wasio waaminifu.
Kauli hiyo ameitoa Septemba 19, 2024 Mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro, wakati
wa hafla fupi ya kukabidhi hati miliki za ardhi 256 kwa Wananchi wa Mtaa wa
Bonite Kata ya Shirimatunda na Wananchi wa Mtaa wa Kariwa chini wanaoishi Kata
ya Rau.
Naibu Waziri Pinda amewatahadharisha wananchi hao kuwa, hati miliki za
ardhi ni nyaraka na mali ambayo haipaswi kuazimishwa kwa mtu yeyote ili
akachukulie mkopo benki, bila kujua utaratibu wa namna ya kurejesha mkopo.
Pia Naibu Waziri Pinda amewasihi wananchi wanapokuwa na migogoro ya
ardhi ni vizuri wakakaa na mabaraza ya familia kwa njia ya usuluhishi na kuacha
kukimbilia mahakamani.
“Mahakama ni chombo kilichowekwa kwa ajili ya kusaidia jambo ambalo
limeshindikana kwenye ngazi ya chini, fedha ambazo mnazitumia kwa ajili ya
kuendeshea kesi mngeweza kuzifanyia kwa shughuli zingine za maendeleo.”amesema.
Aidha amewataka Watumishi wa Sekta ya Ardhi kote nchini, kufungua milango kwa wananchi pindi
wanapofika ofisini kwa ajili ya kupata huduma waweze kuwajibu kwa lugha nzuri.
Akizungumza Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi Mwl.
Mwajuma Nasombe, amesema changamoto zinazoikabili sekta ya ardhi ndani ya Manispaa
hiyo ni pamoja na upungufu wa watumishi katika kada hiyo kulingana na ikama.
Kwa upande wake Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Kilimanjaro Rehema
Mdee, amesema kupitia kliniki za ardhi wananchi wengi wameweza kujitokeza na
kurasimisha maeneo yao na kuweza kuandaliwa hati miliki za ardhi zao.
Katika kikao hicho pia Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya
Makazi Geofrey Pinda, aliweza kusikiliza changamoto na kero za wannanchi ambapo
aliweza kuzitolea majibu ya hapo kwa papo na nyingine akatoa maelekezo kwa
Mamlaka za upangaji Miji.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Geophrey Pinda, Mwenyekiti wa CCM Moshi Mjini Faraji Swai, Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Kilimanjaro Rehema Mdee, Mkurugenzi wa Halmashari ya Manispaa ya Moshi Mwl. Mwajuma Nasombe na Mbunge wa Jimbo la Moshi Vijijini Prof. Patrick Ndakidemi.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi Mwl. Mwajuma Nasombe
Mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini Priscus Tarimo
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Moshi Mjini Faraji Swai
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi Geophrey Pinda
Wananchi wa Kata ya Shirimatunda na Kata ya Rau waliojitokeza kwa ajili ya kupokea Hati Miliki zao za Ardhi, baada ya kukamilisha Urasimishiaji wa maeneo yao.
Naibu Waziri wa Ardhi Geophrey Pinda akimkabidi mmoja wa wananchi wa Kata ya Shirimatunda Hati Miliki yake.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi Mwl. Mwajuma Nasombe, akimkabidhi mkazi wa Mtaa wa Bonite Kata ya Shirimatunda Hati Miliki yake ya Ardhi.
Mkazi wa Mtaa wa Bonite akipokea Hati Miliki ya Ardhi kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM Moshi Mjini Faraji Swai.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Moshi Mjini Faraji Swai, akimkabidhi mmoja wa wakazi wa Kata ya Shirimatunda Hati Miliki yake ya Ardhi.













