Mwenyekiti wa (UWT) Wilaya
ya Moshi Vijijini Ruwaichi Kaale, akimkabidi msaada wa vitu mbalimbali kwa mzee aliyejiweza Stephano Sauli, ikiwa ni Wiki ya Maadhimisho ya Jumuiya hiyo, ambayo
kimkoa ilifanyika katika viwanja vya
Zahanati ya Marry Bennett iliyoko Kata ya Kindi Wilayani humo.
MOSHI-KILIMANJARO
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Wilaya ya Moshi Vijijini Ruwaichi Kaale, ameitaka jamii kuendelea kuwasaidia watu wenye uhitaji ndani ya jamii hata kwa mahitaji madogo, ili kutatua changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo.
Hayo ameyasema septemba 21,2024 wakati akitoa msaada wa vitu mbalimbali kwa watoto yatima pamoja na wazee wasiojiweza wanaoishi Kata ya Kindi, ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya UWT kimkoa ilifanyika katika Viwanja vya Zahanati ya Marry Bennett iliyoko Kata wilayani humo.
Kaale amewaomba Watanzania wenye
uwezo kujitokeza kwa wingi kuwasaidia kwa kile walichojaliwa na Mwenyezi Mungu ili
wasijione kuwa wametengwa na jamii.
“Katika maadhimisho ya Wiki ya UWT tumeweza kutoa misaada mbalimbali kwa wazee wasiojiweza na watoto yatima sambamba na kuotesha miti kwenye maeneo ya taasisi za umma,”amesema Kaale.
Mwenyekiti huyo alitumia fursa hiyo pia kuwahamasisha wanawake wilayani humo, kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwenye uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa ili kuchochea maendeleo hapa nchini.
“Nitoe wito kwa Wanawake wote nchini tuhakikishe tunaunga juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan, kwani ameleta fedha nyingi za maendeleo kwenye kila Mkoa, Wilaya na Kata,"amesema.
Amesema miaka ya nyuma
mtoto alikuwa akifaulu kuwenda sekondari, mzazi alishindwa kumsomesha kutokana
na kutokuwa na fedha, lakini katika kipindi cha Awamu ya Sita ya Uongozi wa
Rais Samia, wazazi wanatembea kifua mbele hawadaiwi tema michango.
“Rais Samia ametoa elimu bila
malipo, mtoto sasa hivi akifaulu anasoma bure ni yeye mwenyewe ashindwe.” Amesema
Kaale.
Kwa upande wake Katibu wa
UWT Mkoa wa Kilimanjaro Irimina Mushongi, amesema katika maadhimisho ya wiki UWT, walishiriki kufaya
usafi nyumba ya mtumishi wilaya ya Moshi mjini, walitembelea wagonjwa hospitali
ya rufaa ya mkoa wa Mawenzi, Zahanati na Vituo vya Afya, pamoja na kupanda miti
zaidi ya 200 lengo likiwa ni katika
kuhifadhi mazingira.
“Tumeweza kuongeza
wanachama UWT 560 na kuwasajili kwenye mfumo, pia tumeweza kuwahamasisha wananchi
kujitokeza kwa wingi kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa, kujiandikishaji kwenye
Daftari la Kudumu la mpiga kura na Daftari la Mkaazi, tumeweza kutoa elimu ya
ukatili wa Kijinsia, lakini pia na kukutana na vikundi vya akina mama, vijana
na watu wenye ulemavu na kutoa elimua ya mikopo.”amesema.
Mwenyekiti wa (UWT) Mkoa wa
Kilimanjaro Elizabeth Minde, akisalimiana na Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Moshi
Vijijini Ruwaichi Kaale, baada ya kuwasili katika Kata ya Kindi. Kwenye
maadhimisho ya wiki ya UWT
Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya
Moshi Vijijini Ruwaichi Kaale, akipanda mti, wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya
UWT Kimkoa iliyofanyika Septemba 21,2024 Kata ya Kindi Wilaya ya Moshi
Vijijini.
Katibu wa UWT Mkoa wa
Kilimanjaro Irimina Mushongi akisalimiana na Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Moshi
Vijijini Ruwaichi Kaale.
Mwenyekiti wa (UWT) mkoa wa
Kilimanjaro Elizabeth Minde (kushoto) akiteta jambo na Mwenyekiti wa UWT Wilaya
ya Moshi Vijijini Ruwaichi Kaale
Mwenyekiti wa (UWT) Wilaya ya Moshi Vijijini Ruwaichi Kaale, akimkabidhi
mmoja wa watoto yatima misaada mbalimbali ya kibinadamuWatoto yatima wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa UWT mara baada ya kukabidhiwa misaada.
Mwenyekiti wa UWT Kata ya
Kindi Pamela Mallya akisalimiana na Mwenyekiti wa UWT Moshi Vijijini Ruwaichi
Kaale, mara baada ya kuwasili katika kata hiyo kwenye maadhimishi ya wiki ya
UWT mkoa wa Kilimanjaro.
Mwenyekiti wa (UWT) mkoani
Kilimanjaro Elizabeth Minde, wa kwanza kushoto,
katikati ni Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Moshi Vijijini Ruwaichi Kaale na
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji UWT Mkoa wa Kilimanjaro Mwl. Lightiness Malula,
wakiwa na zawadi kwa ajili ya kuwakabidhi wazee na watoto yatima.
Maria John wa kwanza kushoto, Joseph Barnaba, Bakari
Massawe na Stephano Sauli, wakiwa wamepakata zawadi mbalimbali walizokabisdhiwa
na UWT mkoa wa Kilimanjaro.
Wanawake wasiojiweza wakiwa
katika picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa misaada mbalimbali ya kibinadamu na
viongozi wa UWT, kwenye maadhimisho ya Wiki ya UWT kimkoa yaliyofanyika Kata ya
Kindi Halmashauri ya Wilaya ya Moshi Vijijini.
