KINDI- MOSHI
JUMUIYA ya Umoja wa Wanawake Tanzania wa Chama cha Mapinduzi (UWT) Mkoani Kilimanjaro umesema hauko tayari kuyumbumbishwa na kuacha ajenda yao inayolenga kumchagua Rais Samia Suluhu Hassan katika uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika nchini mwakani.
Hayo yameelezwa Septemba
21,2024 na Mwenyekiti wa UWT mkoani Kilimanjaro Elizabeth Minde, wakati wa Wiki
ya Maadhimisho ya wiki ya UWT, Mkoa wa Kilimanjaro yaliyofanyikia katika
Zahanati ya Marry Bennett iliyoko Kata ya Kindi, Halmashauri ya Wilaya ya
Moshi, Mkoani humo.
“Sisi ajenda yetu hiyo ni
kutembea na Mama ambaye ni Rais Samia Suluhu Hassani, kwa maana yakuhakikisha
anachaguliwa tena kuendelea kuiongoza nchi baada ya mafanikio makubwa tuliyoyapata
baada ya kushika wadhifa huo miaka mitatu iliyopita”, alisema Minde.
Minde alisema kuwa ili Umoja
huo ufanikiwe kutekeleza azma hiyo ni vyema wanawake wote wakaungana na kukata
hila zote zitakazowasilishwa zenye kumkwamisha Rais Samia kuendelea na kazi
nzuri anazofanya.
“Tunapozungumzia ajenda ya
Rais Mwanamke ni ajenda inayolenga maendeleo; tumeshuhudia katika miaka mitatu
ya utawala wake Rais Samia Suluhu Hassan, amefanya kazi nyingi zikiwemo zile za
kumtua Mama ndoo kichwani pampja na wanawake kuaminiwa kushika nafasi
mbalimbali za uongozi na hivyo kuondoa mfumo dume uliokuwa kwenye nyanja za
uongozi hapa nchini”, alisema.
Alisema kipindi kilichopita
mwanamke aliachwa nyuma kwa kigezo kuwa hana elimu, lakini kwa sasa wengi
wameaminiwa kushika nyadhifa mbalimbali na wamefanya na wanaendelea kufanya
kazi nzuri.
“Wanawake tusiruhusu
jitihada anazofanya Rais Samia kupitia utendaji wake mzuri serikalini yeye
pamoja na wenzake badala yake tuunganishe nguvu zetu kwa pamoja ili kuhakikisha
anaendelea kutekeleza majukumu yake kwa manufaa ya nchi”, alisema.
Kwa upande wake Mwenyekiti
wa (UWT) Wilaya ya Moshi Vijijini Ruwaichi Kaale, ametoa wito kwa wanawake kujitokeza
kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la mkazi tayari kushiriki kwenye
uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.
“Pia nitoe rai kwa Wanawake kujitokeza wakati wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la mpiga kura tayari kwa ajili ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwakani”, alisema.
Aidha aliwataka Wanawake
kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi mbalimbali wakati wa uchaguzi wa Serikali
za Mitaaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu.
Kaale pia alitoa rai
kwa Wanawake kuhakikisha wanatangaza
kazi nzuri alizofanya Rais Samia Suluhu Hassan, ikiwemo kuboresha huduma za
afya, elimu, miundombinu ya barabara, umeme pamoja na sekta ya maji hapa nchini
na hivyo kuwahakikishia wananchi maisha bora.
Awali akizunguimza Katibu
wa UWT Mkoa wa Kilimanjaro Irimina Mushongi alisema kuwa katika kuadhimisha
wiki hiyo, UWT ilifanya shughuli mbalimbali ikiwemo kufanya matendo ya huruma
na kuboresha mazingira.
“Tumetembelea hospitali ya
rufaa ya mkoa Mawenzi na kutoa misaada aina mbalimbali, pia tumetoa misaada kwa
wazee wasiojiweza wanaishi Kata ya kindi pamoja na watoto yatima”, alisema
Mushongi.
Aidha alisema pia umoja wa
UWT mkoa ulishiriki katika shughuli za upandaji miti ambapo zaidi ya miti 2,000
imepandwa kwenye zahanati na vituo vya afya na maeneo mengine mbalimbali
ikiwemo kwenye taasisi zinazotoa huduma za elimu.
Wanawake wa UWT Wilaya ya Moshi Vijijini waliojitokeza kuadhimisha Wiki ya UWT Mkoa wa Kilimanjaro iliyofanyika Kata ya Kindi Halmashauri ya Moshi Vijijini.
Wanawake wa UWT Wilaya ya Moshi Vijijini wakitabasamu
Wazee wakiwa wanafuatilia kwa makini hotuba ya Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Kilimanjaro
Viongozi wa UWT Mkoa na Wilaya ya Moshi Vijijini wakiwapungia mikono ishara ya kuwasalimia Wanachama wa UWT Kata ya Kindi hawapo katika picha, waliojitokeza kuadhimisha Wiki ya UWT iliyofanyika Wilaya ya Moshi Vijijini.
Viongozi wa UTW Kata ya Kindi wakiwa katika Maadhimisho ya Wiki ya UWT Mkoa wa Kilimanjaro yaliyofanyika septemba 21,2024 Kata ya Kindi.
Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Kilimanjaro Elizabeth Minde, Mwenyekiti wa UWT Moshi Vijijini Ruwaichi Kaale, Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji Mkoa wa Kilimanjaro Mwl. Lightness Malula na Katibu wa UWT Mkoa wa Kilimanjaro Irimina Mushongi,wakiwa wamebeba zawadi kwa ajili ya kuwakabidhi watoto yatima na wazee.
Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Kilimanjaro Elizabeth Minde akimkabidhi mmoja wa watoto yatima zawadi, ikiwa ni maadhimisho ya Wiki ya UWT
Mwenyekiti wa UWT Kata ya Kindi Pamela Mallya akimkabidi mzeePaulo Leina zawadi
Katibu wa UWT Mkoa wa Kilimanjaro Irimina Mushongi, akimkabidhi misaada ya kibinadamu Mzee Joseph Barnaba, kwenye Wiki ya Maadhimisho ya UWT Mkoa wa Kilimanjaro.
Diwani wa Viti Maalum Kata ya Kirima Aurelia Mushi, akimkabidhi sukari, mchele na mche wa sabuni ya kufulia mmoja wa wazee, ikiwa ni Maadhimisho ya Wiki ya UWT.
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya UWT Wilaya ya Moshi Vijijini Asha Abdallah akimkabidhi mmoja wa wazee sabuni za kufulia ikiwa ni Maadhimisho ya Wiki ya UWT yaliyofanyika Septemba 21,2024 Kata ya Kindi.
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji Wilaya ya Moshi Vijijini, akimkabidhi mmoja wa wazee zawadi zilizotolewa na UWT katika kuadhimishi wiki ya UWT
Mwenyekiti wa CCM Kata ya kindi Juma Abdulrahman Mwisi, akimkabidhi zawadi mmoja wa wazee wakati wa Maadhimishi ya Wiki ya UWT.
Viongozi wa UWT Wilaya ya Moshi Vijijini wakimkabidhi zawadi mbalimbali mmoja wa watoto yatima ikiwa ni Maadhimisho ya Wiki ya UWT Kimkoa yaliyofanyika Wilaya ya Moshi Vijijini.
Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Kilimanjaro Elizabeth Minde, akisalimiana na akina Mama wa UWT Kata ya Kindi.
Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Kilimanjaro Elizabeth Minde (kushoto) akimlisha kipande cha keki Mwenyekiti wa UWT Moshi Vijijini Ruwaichi Kaale, wakati wa Maadhimisho ya UWT Kikoa yaliyofanyika Wilaya ya Moshi Vijijini Septemba 21,2024.
Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Moshi Vijijini Ruwaichi Kaale, akizungumza na Wanawake wa Jumuiya hiyo, mara baada ya kumalizika kwa maadhimisho ya Wiki ya UWT Kimkoa yaliyofanyika katika Viwanja vya Zahanati ya Marry Bennett iliyoko Kata ya Kindi Wilayani ya Moshi Vijijini.

















