Wafanyabiashara wote, waliounguliwa
meza na bidhaa zao kwenye tukio la moto uliotokea Februari 5, mwaka 2020 na
kuteketeza soko la Mbuyuni lililopo Kata ya Bondeni Halmasahuri ya Manispaa ya
Moshi, watajumuishwa kwenye mpango wa kupatiwa vyumba “Flemu” kwenye mradi wa jengo
jipya la soko hilo.
Mwenyekiti wa CCM
Wilaya ya Moshi Mjini Faraji Swai, aliyasema hayo Septemba 25,2024 wakati
Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ilipotembelea na kuangalia mradi
wa ujenzi wa soko jipya la Mbuyuni, unaotekelezwa na Mkandarasi Rocktronic Ltd
kwa gharama ya Sh bilioni 1.6 na kuzungumza na wafanyabiashara wa soko hilo.
Swai amesema, soko la
mbuyuni ni moja ya masoko makubwa na makongwe yaliyopo katika mkoa wa
Kilimanjaro, ambalo linahudumia wafanyabiashara kutoka maeneo mbalimbali.
“Februari 5, 2024
mwaka huu soko hili liliteketea kwa moto na kuacha wafanyabiashara takribani 2,500
wakiwa hawajui la kufanya baada ya bidhaa zao zote kuteketea kwa moto.”amesema.
Moto huo ambao ulioanza
kuwaka majira ya saa sita usiku wa kuamkia Februari 6,2024 huku chanzo chake
kikidaiwa kusababishwa na hitilafu ya umeme.
Ameongeza kusema kuwa
soko hilo lina wafanyabiashara wakubwa, wadogo na wachuuzi wanaonufaika nalo
kati ya Sh 20,000 hadi 50,000 kwa siku, limekuwa ni kiungo muhimu cha biashara
kwa Wajasiriamali wadogo ndani ya Manispaa hiyo.