MOSHI-KILIMANJARO.
Serikali inakadiria
kutumia kiasi cha Sh Bilioni 1.6 kwa ajili ya ujenzi wa soko jipya la Mbuyuni
lililopo Halmashauri ya Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro.
Akitoa taarifa kwa
Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kilimanjaro iliyotembelea
na kukagua ujenzi wa soko hilo Septemba 25,2024 Mkurugenzi mtendaji Halmashuri
ya Manispaa ya Moshi Mwl. Mwajuma Nasombe, amesema kwa kutambua umuhimu wa soko hilo, Baraza la Madiwani, liliitisha kikao cha dharura yakiwa ni maelekezo ya Mkuu wa
mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu, kuona namna ya kutumia mapato ya ndani kwa ajili ya kuanza kujenga soko
hilo.
Nasombe amesema soko
hilo tayari limeanza kujengwa kwa gharama ya Sh Bilioni 1.6 ambapo halmashauri kupitia
mapato yake ya ndani ilitenga Sh Milioni 800 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa soko hilo na kati ya fedha hizo Mkandarasi ameshalipwa Sh milioni 238.
“Huko nyuma soko hilo,
lilijengwa kwa tofali za udongo, kwa sasa soko linakwenda kujengwa kwa tofali
za bloku na kuwekewa slabu chini, maduka 14, matundu ya vyoo 16, kupauliwa pamoja na miundombinu ya mifereji ya maji kuzunguka
soko na.”amesema
Akizungumza Meya wa
Manispaa ya Moshi Mhandisi Zuberi Kidumo, amesema Baraza la Madiwani kwa pamoja, walikubaliana kusimamisha miradi mingine yote iliyokuwa inatekelezwa kwenye kata zao ili soko hilo lijengwa
kwa wakati.
Naye Mbunge wa Moshi Mjini Priscus Tarimo amesema “Soko la Mbuyuni ni eneo muhimu kwa maendeleo ya wakazi wa Moshi mjini na viunga vyake, vikiwemo vijiji vya Shabaha, Mabogini na Mailisita vinavyotegemea huduma kwenye soko hilo.
Awalia Mwenyeki
wa soko la Mbuyuni Lameck Mziray, amesema ataendelea kusimamia maelekezo ya
viongozi wa chama na Serikali kuhakikishan Wafanyabiashara wote waliokuwa
kwenye soko hilo kabla ya kuungua wanarudi kwenye maeneo yao.
Kwa upande wake
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro Patrick Boisafi, amewahakikishia kila
mfanyabiashara wa soko la Mbuyuni, aliyekuwa akifanya biashara katika soko hilo
atarudi bila kutoa shilingi moja.