MOSHI-KILIMANJARO
Wanawake waliopo
kwenye mahusiano na ndoa wametakiwa kuacha kuvigeuza vyumba vya kulala kuwa ni
vyumba vya mahakama.
Hayo yamesemwa Septemba
5,2024 na Mwanasaikolojia Tiba na Ushauri Nasihi Edna Ngowi, wakati
akizungumza na waandishi wa habari kwenye kongamano la Watoto Mentorship
Adventure, iliyoandaliwa na Shirika lisilo kuwa la kiserikali la Inspire
Change.
Ngowi amesema
wako baadhi ya wanawake wamekifanya chumba cha kulala kuwa ni (Court
Room) chumba cha mahakama, kugombana pindi mume wake anaporudi nyumbani.
Amesema sababu ya wanaume kuchelewa kurudi nyumbani na kaumua kurejea wakati wa kula na kulala ni kwamba anajua akifika mapema nyumbani ataanza kugombezwa jambo ambalo wanaume hawpendi.
“Wanaume wengi wanarudi saa nne za usiku ni kutokana na kugombezwa hata anapokuwa chumbani amepumzia, chumba hicho kinageuka na kuwa chumba kugombana na hizo ndio sababu ambazo humfanya mwanaume kuona ni bora kupiga piga stori na marafiki zake ili akifika nyumbani ni kula na kulala tu.
“Kwenye vitabu
vitakatifu vinatueleza kwamba Mwanaume ndio kichwa cha nyumba hata awe mwanaume
ambaye hawezi kumudu nyumba yake, lakini bado mke unatakiwa kumheshimu kama
baba mwenye nyumba, hata kama mali Mungu amekupa kuliko ya mume wako ni Mungu
ameamua apitishe kwenye mkono wako wewe mke, kwani zile ni baraka za Mungu
mnatakiwa mzitumie wote , kwa kuheshimiana na kupendana.
Aidha Mtaalamu huyo amesema kutokana na ugomvi pamoja na kelele za mara kwa mara ndani ya familia, zinachangia hata watoto kuwa na msongo wa mawazo na kutoa wito kwa wana ndoa hao ni muhimu kuzungumza kwa upendo ili kutatua matatizo hao ili kuweza kujenga uhusiano wenye afya njema.
Kwa upande wake mkufunzi na mboreshaji wa afya ya Jamii Dkt.
Sabina Mtweve, amesema changamoto inayo waathiri watoto wengi kiafya kwa sasa
ni kutumia muda mwingi ni kucheza gemu pamoja na kuangalia picha chafu mitandaoni,
jambo ambalo linasababisha hata uwezo wao wa kudadisi unapungua kutokana na
kupata taarifa mbalimbali kuingia kwenye akili zao.


