MOSHI-KILIMANJARO
Kampuni
ya Pamoja Occasion Organisers Limited ya Mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro,
imezindua vinywaji baridi vinavyotokana na zao la Kahawa.
Uzinduzi wa kinywaji hicho ulifanyika Septemba 9,2024, ambapo ulioenda sambamba na
uzinduzi wa Tamasha la tano la msimu wa Kahawa (Kahawa Festval-2024) uliofanyika katika
ukumbi wa mnada wa Bodi ya Kahawa Tanzania TCB.
Akizungumza katika hafla hiyo ya uzinduzi Mkurugenzi wa Kampuni ya Pamoja Occasion Organisers Limited Vicent Mulungwana, amesema utengenezajia wa kinywaji cha kahawa baridi, umeongeza mahitaji ya watu kukitumia kinywaji hicho huku akisema kuwa, wengi ambao walikuwa wanakataa kukitumia kinywaji hicho kwa sasa wamekuwa kimbilio la bidha hiyo kutokana na ladha yake kuwa nzuri.
"Kinywaji hiki kinatumiwa na watu wote kuanzia mtoto mdogo hadi watu wazima, watu wanapo tumia kinywaji hiki ambazo mtumiaji anaweza kuzipata ikiwemo kukabiliana na maradhi mbalimbali kama vile saratani, maradhi ya moyo, kiharusi pamoja na kuondoa magonjwa ya uzee na hivyo kumfanya mtu huyo aweze kuishi maisha marefu."amesema.
Anazitaja zaida zingine zitokanazo na unywaji wa kahawa huo kuwa, mbali na kupoteza kumbukumbu pia hulinda afya ya ini, huondoa msongo wa mawazo, na hukabiliana na maradhi mbalimbali.
Amesema tu yeyote anayetumia kahawa hiyo baridi kwanza inamsaidia kwenye mwili wake kupata mzunguko wa damu kukaa vizuri pia ina muwezesha kupata joto la mwili na joto la damu kukaa sawa,
Vilevile ina msaidia kutokuugua vidonda vya tumbo, kurejesha kumbukumbu kwenye kongosho lakini pia inakwenda kusafisha mafuta ambayo yanakuwa yamejikusanya juu ya utumbo na hivyo kumsaidia kula chakula vizuri na kunywa maji kwa wingi hivyo kuufanya mzunguko wake wa damu kuwa sawa.
Katika hatua nyingine Mlungwana ameipongeza Bodi ya Kahawa Tanzania (TCB) kwa
kuendelea kuwahamasisha Watanzania kuongeza hamasa ya unywaji wa kahawa ili
kuboresha afya zao sambamba na kuimarisha soko la ndani la zao hilo.
“Kutokana na TCB kuendelea,
kuwahamasisha Watanzania kunywa kahawa ya ndani kwa sasa kuna mabadiliko
makubwa ya wananchi kutumia bidhaa za ndani zinazotokana na zao la kahawa.”amesema,
Akizindua msimu wa tano wa
Tamasha la Khawa (Kahawa Festival-2024) Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nurdin,
ameipongeza Kampuni ya Pamoja Occasion Organisers Limited kwa kutengeneza
kinywaji hicho ambacho kitakwenda kuongeza unywaji wa kahawa wa ndani.
“Kahawa ni zao la kiuchumi
na tegemezi kwa Mkoa wa Kilimanjaro na nchi kwa ujumla, hivyo utamaduni na
desturi ya unywaji wa kahawa utaimarisha sana soko letu la ndani na kupunguza
utegemezi kwenye soko la kimataifa kwani bei inapoyumba katika soko la dunia
huathiri moja kwa moja pato na uchumi wa mkulima na Serikali kwa ujumla.”amesema
Babu.




