HeavenLight Kiondo: atimiza ndoto ya kuwaunganisha wajane

MOSHI-KILIMANJARO.

Wanawake Wajane wanaoishi Kata ya Korongoni Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro wamempongeza Diwani wa kata hiyo HeavenLight Kiondo kwa uamuzi wake wa kukutana na kubadilishana nao mawazo.

Wakizungumza baada ya mkutano huo na kusikiliza changamoto wanazozipitia baada ya kuondokewa na wenzi wao, Betty Maimu na Hindu Ally, wamesema suala hilo halina budi kuigwa na viongozi wengine.

Wamesema amefurahishwa na diwani wa kata ya Korongoni kwa kuwakutanisha na kula nao chakula jambo ambalo limewapa faraja kubwa kwao.

Akizungumzia changamoto wanazo kumbana nazo Matilda Mawalla na Judith Kundi wamesema kuwa wajane wanakumbana na changamoto nyingi punde wanapoondokewa na wenzi wao ikiwemo ile inayohusiana na maswala ya ufuatiliaji wa miradhi. 

Wamesema matatizo ya wajane huanza pale wenzi wao wanapofariki na kwamba uamuzi wa Diwani Kiondo ni msingi mzuri wa wanawake wajane kuanza kufuatilia haki zao za msingi zinazohusiana na mirathi ya marehemu waume zao.

Naye Kabibu wa Baraza la wazee Kata ya Koriongoni Hilda Mlay, amesema Wanawake  wajane wamekuwa wakipitia changamoto nyingi na kuiomba serikali kuliangali suala hilo ili waweze kupata haki zao kwa wakati.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Korongoni HeavenLight Kiondo amesema, amekuwa akipitia changamoto nyingi kama mwanamke kiongozi.

“Nimekuwa nikipitia changamoto nyingi kubwa sana kama mwanamke kiongozi, wakati mwingi nimekuwa nikifanya ibada ya kuomba na wako hapa wajane nikiwashirikisha kuniombea,”amesema Diwani Kiyondo.

Naye Mbunge wa Jimbo la Moshi Priscus Tarimo amempongeza Diwani Kiondo kwa uamuzi wa kuwakutana wajane hao na kueleza hatua hiyo imefungua ukarasa mpya utakaowawezesha kufuatilia haki zao.

Akizungumza Katibu wa Siasa na Uenezi Moshi Mjini Athumani Ally Mfutu, ametoa wito kwa wanawake wajane kujiunga kwenye vikundi vya ujasiliamali ili waweze kunufaika na mikopo inayotolewa na Serikali bila riba.














 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.