SAME-KILIMANJARO
Halmashauri ya Wilaya ya same imekabidhi pikipiki kwa watendaji wa kata
ili kuwarahisishia ukusanyaji wa mapato, huku ikiwaonya watendaji hao
kutozigeuza pikipiki hizo kuwa bodaboda.
Onyo hilo limetolewa Agosti 28,2024 na Mwenyekiti wa Halmashari hiyo
Yusto Mapande, wakati akikabidhi pikipiki hizo
kwa maofisa watendaji wa kata tatu za Miamba, Chome na
Vudee ambazo ziko ukanda wa milimani.
Amesema kuwa pikipiki hizo
ambazo zimegaiwa ni mali ya Halmashauri hivyo mtendaji yeyote akipatikana
anafanya biashara ya bodaboda tofauti na
matumizi ambayo yamekusudiwa hawatasita kuzichukua na kuzipeleka sehemu
nyingine kwa watendaji wa kata ambao
hawana usafiri huo.
“Watendaji wa kata
tuliowakabidhi pikipiki hizi hakikisheni mnavitumia vyombo hivi kwa malengo
yaliyokusudiwa na wale ambao watakwenda kinyume tutawanyang’anya pikipiki hizi
na kuwapa watendaji wengine wenye uhitaji,”amesema Mapande.
Amesema pikipiki hizo wamezikabidhi kwa watendaji kwa lengo la kwenda
kuongeza kasi ya ukusayaji wa mapato na usimamizi wa miradi ya maendeleo pamoja
na kuongeza uwajibikaji kwa kutatua kero mbalimbali wananchi kwenye kata zao.
Akizungumza kwa niaba ya mtendaji
kata ya Miamba Diwani wa Kata hiyo Greyson Kiondo Fue, ameishukuru Halmashauri
hiyo kwa kuwagaiwia pikipiki hizo jambo ambalo litawasaidia katika utekelezaji
wa majukumu yao.
“Tunaishukuru sana serikali imetusaidia kutuwezesha nyenzo muhimu ya
usafiri wa pikipiki kwasababu awali tulikuwa tunapata changamoto kubwa ya
umbali wa maeneo katika ukusanyaji wa mapato pamoja na ufuatiliaji wa miradi
kutokana na jiografia ya maeneo yetu ya milimani,”amesema.
Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Same Amosi
Kusakula, amesisitiza Watendaji kuhakikisha wanakwenda kutatua kero za
wananchi.
“Changamoto na migogoro mingi inayotokea, mingi inasababishwa na baadhi
ya uzembe wa watendaji ndani ya serikali, sisi kama viongozi wa chama ni vizuri
tukaiambi
Aidha amesema viongozi wa serikali kuwajibika kwenye chama tawala si
hisani bali ni matakwa ya kikatiba, hivyo wanao wajibu wa kutoka ofisini na
kwenda kutatua changamoto za wananchi na waondoe dhana kwamba hiyo ni kazi ya
vyama vya siasa.
MWISHO.