Benki ya NMB yatoa mafunzo kwa wastaafu namna ya kutengeneza kipato badala ya kutegemea pensheni

Benki ya NMB imetoa mafunzo kwa Wastaafu na Wastaafu watarajiwa namna ya kutengeneza kipato chao, badala ya kutegemea pensheni ya kila mwezi ambayo hutolewa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) ili kuendesha maisha yao ya kila siku.

Meneja mwandamizi kutoka Idara ya Wateja Binafsi katika Benki ya NMB Queen Kinyamagoha, ameyasema hayo Agosti 5,2024, wakati wa ufunguzi wa semina ya siku moja kwa wastaafu hao, iliyofanyika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro na kuhudhuriwa na wastaafu zaidi ya 200 kutoka Wilaya ya Moshi Mjini na Vijijini.

Amesema katika semina hiyo wastaafu hao wanakwenda kufundishwa namna mbalimbali za wao wenyewe kuweza kutengeneza kipato kingine, tofauti na kuendelea kusubiria pensheni ambayo huipata kila mwisho wa mwezi ili iweze kuwasaidia.

Amesema Benki ya NMB imeona kuwapa mbinu ya kuishi baada ya kustaafu kwao ikiwemo kuwa na matumizi mazuri ya fedha ,kufanya ufugaji, kilimo na uwekezaji salama na kuepuka matapeli.

Meneja huyo amesema kupitia programu yenye Kaulli mbiu ya HEKIMA PLAN "StaafuKifahari Benki ya NMB imeona kuja na utaratibu huo ili kuenzi mchango mkubwa wa watumishi hao katika ujenzi wa taifa.

Kinyamagoha amewasihi wastaafu hao kupunguza baadhi ya matumizi yasiyokuwa ya lazima sambamba na kuwa na bajeti ili kuzidi kujiwekea akiba ya mafao waliyoyapata baada ya kustaafu kwao.

Baadhi ya wastaafu akiwemo Celina Masegese na Edward Malisa wamesema, changamoto zinazowakumbwa baada ya wazee kustaafu ni pale ambapo familia zinakuwa zikiwategemea kwa kila jambo, kwa kumuona mstaafu huyo tayari ana mafao ya uzeeni na kujikuta akitumia fedha zote na kushindwa kufikia malengo ambayo alikuwa ameyakusudia.

Mstaafu mwingine Mwl. Ally Omar Mhando, amesema kupungua kwa kipato ambacho alikuwa anakipata mstaafu huyo wakati akiwa kazini kumewasababisha baadhi yao kukumbwa na changamoto ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza.

"Changamoto nyingine ni ile ya ndugu kumgeuza mstaafu huyu kuwa ATM yao ya kila tatizo linapotookea katika familia hiyo ili aweze kuwasaidia na hivyo kujikuta akiwa ameishiwa kile alichokipata kutoka kustaafu kwake.








Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.