Watanzania wahamasishwa kutumia bidhaa za ngozi zinazozalishwa na wazalendo

Mkurugenzi wa Kiwanda cha kutengeneza bidhaa za ngozi Michael Gadi Uronu, akionesha moja ya bidhaa ya ngozi aina ya begi, anayoitengeneza katika kiwanda chake. Muonekano wa bidhaa za mazao yatokanayo na ngozi, anazozitengeneza kwenye kiwanda chake cha ngozi cha Uronu Leather Craft, kilichoko Moshi Mjini mkoani Kilimanjaro. (Picha na: KISENA)


Watanzania wametakiwa kujenga utamaduni wa kununua bidhaa ngozi zinazozalishwa nchini ili kutoa fursa ya masoko ya uhakika kwa wazalishaji wa bidhaa hizo hapa nchini.

Mkurugenzi wa kiwanda cha kutengeneza bidhaa za ngozi mjini Moshi cha (Uronu Leather Craft) Michael Uronu, aliyasema hayo jana, wakati akizungumza na Tanzania Leo, katika mohojiano maalumu mjini humo.

Amesema unafuu wa bidhaa zinazotoka nje ya nchi ni miongoni mwa mwa sababu anazozitaja kuwafanya baadhi ya Watannzania kuchangamkia bidhaa hizo kuliko zinazozalishwa ndani ya nchi.

“Tanzania ina viwanda vinavyotengeneza bidhaa nzuri zisizo kuwa na mashaka, bidhaa zinazotengenezwa nchi zina viwango vyote vinavyotakiwa na taasisi za ukaguzi, hivyo Watanzania ninawahamasisha kujenga utamadunia wa kununua bidhaa zetu za ndani,”amesema.

amesema “Bidhaa za ngozi ni bora na ni imara zaidi, niwaombe Watanzania wenzangukutumia bidha zetu za ngozi ambazo tunazitengeneza hapa ndani, mimi mwenyewe licha ya kuzitengeneza lakini pia ni muumini mzuri wakuzitumia bidhaa hizi za ngozi, kwanza ni imara, niwaombe waweze kuachana na kukimbilia vitu vya plasitiki kwa unafuu wa bei."

Amesema wako baadhi ya watanzia wamezoea kununua bidhaa za mabegi ya kichina kutoka nje ya nchi, ambayo unakuta ni bei rahisi na wanapolinunua ndani ya wiki mbili au mwezi mmoja linakatika na kurudi tena kununua jingine, lakini kama wangenunua begi la ngozi wanaweza kudumu nalo kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Uronu amesema pamoja na kiwanda chake kutengeneza bidhaa za ngozi pia ameweza kutoa fursa za ajira za moja kwa moja kwa vijana watano, huku akiiomba serikali kuwaunga mkono zaidi ili kujenga uchumi imara kupitia Sekta ya ngozi.

“Katika juhudi za kuunga mkono Serikali ya uchumi wa viwanda, kuna haja kwa Watanzania kujenga utamaduni wa kununua bidhaa zinazozalishwa nchini ili kutoa fursa zaidi ya masoko ya ngozi nchini.”amesema Uronu.

Kwa upande wake Fundi mkuu wa kiwanda cha (Uronu Leather Craft) Muhsiwi Ali Hoza anesema, changamoto ya bidhaa za ngozi umethiriwa zaidi na uingizwaji wa bidhaa za plasiti kutoka nje ya nchi.

“Bidhaa za plasiti ambazo zinatoka nje ya nchi kama vile kama vile mabegi, mikanda, pochi na mikoba, inaathiri zaidi soko la bidhaa za ndani za ngozi , mtu anakimbilia zaidi kunua bidhaa hizo kutokana na urahisi wa bei.”amesema Hoza.

Aidha changamoto nyingine ambayo anaiona kwenye viwanda vya ngozi, ni namna ya utengenezaji wa bidhaa hizo huku akishauri kuweza kutengeneza bidhaa iliyo bora ili kuendana na soko lililopo kwa sasa.

“Ngozi za ndani zinakuwa kavu sana, ukilinganisha na ngozi kutoka Kenya, Ethiopia na Italia zinakuwa na mafuta, tunawaomba wenye viwanda kutengeneza ngozi zenye viwango ili kuweza kushindana katika masoko.

Kwa mujibu wa Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdalah Ulega, amenukuliwa na vyombo vya habari akiwahamasisha Watanzania kujenga utamaduni wa kupenda kununua bidhaa za ndani na hasa bidhaa zinazotokana na mazao ya ngozi huku ikiweka wazi mikakati yake katika kuhakikisha ngozi za Tanzania zinaendelea kuwa bora.

Ulega, anasema ipo haja ya Watanzania kuhakikisha wananunua bidhaa zitokanazo na mazao ya ngozi ambazo zinatengenezwa na viwanda vya ndani ya nchi badala ya kununua bidhaa za ngozi zinazotoka nchi nyingine.

Aidha Waziri Ulenga anasema kuwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha ngozi ambayo inatokana na mifugo iliyopo nchini Tanzania inaendelea kuwa bora ambapo amefafanua umefika wakati wa kuhakikisha ng'ombe wanaandaliwa tangu wanapozaliwa ngozi yao inalindwa ili iwe bora zaidi na hiyo si tu itafanya kuwepo na ngozi bora bali kuongeza thamani ya ngozi na bidhaa zake.

Kuhusu soko la bidhaa zitokanazo na ngozi, anasema Wizara hiyo, inawahakikisha wadau wa ngozi kuwa Serikali imejipanga katika kuhakikisha kunakuwa na soko la uhakika ambapo ameahidi kuendelea kufanya mazungumzo na Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na wadau wengine kwani dhamira ya Serikali ni kujenga viwanda na hivyo kuna kila sababu ya uwepo wa viwanda vya ngozi.

"Tutahakikisha tunakuwa na soko la uhakika katika bidhaa za ngozi hasa katika kipindi hiki cha ujenzi wa viwanda ambapo tunataka kuwepo na viwanda vya bidha za ngozi."
Fundi mkuu wa kutengeneza bidhaa za ngozi Ustath Muhsiwi Ali Hoza,akiendelea na shughuli za ushonaji wa bidhaa za ngozi. (Picha na: KISENA)








Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.