Katibu wa Kamati ya Mashindano ya Zuberi Cup 2024 Pascal Mhere.
● Ukiwa ni msimu wa nne toka kuanzishwa kwa mashindano hayo mwaka 2020.
● Tumeanza hatua ya 16 bora , timu takribani 16 ambazo zimepata nafasi ya kufika hatu ya hiyo kati ya zile timu 44.
● Timu hizo zimeanza Julai 20, 2024 kwa mchezo ambao umezikutanisha timu ya Msaranga FC na Timu ya Badland FC ambazo zimefungua dimba la kucheza , na kumalizika kwa Msaranga kuibuka na ushindi wa 2-0 lakini pia kutakuwa na michezo mingine hadi Julai 27 mwaka huu.
● Tangu kuanza kwa mashindano hayo tumeshuhudia ushindani mkubwa umezidi kuonekana kati ya timu moja hadi nyingine.
● Tuna washukuru wadau mbalimbali ambao wameendelea kuona thamani ya mashindano hayo wakiwemo AZANIA BANK ambao wameona kunanhaja ya kuongeza nguvu katika maahindano hayo.
● Wamejitolea kutoa zawadi ya mchezaji bora kila mchezo utakaokuwa ukichezwa, pia watatoa zawadi kwa golikipa , mshambuliaji bora, mchezaji bora wa mashindano na watatoa pia na zawadi kwa kikundi cha uhamasishaji.