Soko la Mazao kujengwa Kileo, Mwanga

MWANGA, KILIMANJARO

Wizara ya Kilimo inatarajia kuanzisha ushirikiano na Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Mkoani Kilimanjaro, kwa ajili ya kujenga soko la mazao ya kilimo, ambalo litakuwa na sehemu ya kuhifadhia na kuuzia mazao ya wakulima hao.

Mbunge wa Jimbo la Mwanga Joseph Tadayo, ameyasema hayo kwenye mkutano wa hadhara na wananchi wa  kijiji cha Kituri, uliofanyika katika Ofisi ya Serikali ya Kijiji hicho, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kupokea changamoto mbalimbali zinazo wakabili wananchi katika maeneo yao.

“Ziko fedha ambazo zimetolewa na Wafadhi kupitia Wizara ya Kilimo, ambazo zinakwenda  kujenga masoko ya mazao ya kilimo na miongoni mwa masoko hayo yatakayojengwa moja liytajengwa hapa kijiji cha Kituri.”amesema.

 Tadayo amesema kujengwa kwa saoko hilo wananchi watapata fursa ya kuuza mazao yao hapo, ambapo  kutakuwa na maghala pia ya kuhifadhia  mazao yao, mkulima atakapo kuja na mazao yake na yasiweze kupata wanunuzi  atayahifhadi kwenye maghala hayo.

“Lengo langu  hii  Kata ya Kileo iweze kuwa kama Kibaigwa kwa sababu hapa ni eneo la Center, watu kutoka Kenya watakuja hapa na kununua mazao ya wakulima na Serikali itaweza kupata mapato yake”amesema Mbunge Tadayo.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Kileo Kuria Msuya, amesema kujengwa kwa soko la mazao ya kilimo katika kata hiyo , litakwenda kuongeza thamani ya bidhaa za wakulima  kutoka mashambani.

“Ziara ya Mbunge imenipa faraja kubwa kama kiongozi wa Kata, amekuja na habari njema inayohusiana na ujenzi wa soko la mazo ya kilimo, kwa ajili ya kupandisha thamani bidhaa za wakulima kutoka mashambani.”amesema DIwani Kuria.

Ameongeza kuwa “Kata ya Kileo ina jumla ya hekta 2,400 ambazo zinafaa kulimwa kwa kipindi chote cha mwaka mzima na kijiji cha Kivulini kina jumla ya hekta 1,050 ambapo, hekta zinazotumika kwa kilimo ni hekta 400 tu.”

Kuria amesema kilio cha wananchi wa Kata hiyo ni kupata soko la pamoja la kuuzia mazao yao ya kilimo, serikali kujenga soko hapa litakwenda kuongeza uchumi wa wakulima na wananchi wa wilaya ya Mwanga kwa ujumla, jambo ambalo litakwenda kuwaondoa walanguzi.

Mkazi wa kijiji cha Kituri Abubakar Kipingu, ameipongeza serikali kwa hatua hiyo ya kuwajengea soko la mazao ya kilimo, kwani litakwenda kuondoa changamoto ya kulanguliwa mazao yao na kupewa bei ya chini ambayo walikuwa hawanufaiki na kilimo hicho kutokana na madalali kulanguliwa.

“Kama Serikali itajengea soko mahali hapa,  vijana tutaweza kujipatia ajira, wakati wakulima wanapouza mazao yao tutaweza kubeba mizigo na kuipakiza kwenye malori na kujipatia ujira wetu,”amesema Ismail Kanyika.

Naye Richard Mchomvu; amesema mkulima analazimika kuuza mazao yake kwa bei yoyote, ili aweze kumpeleka mtoto shule,  kulipa kodi ya nyumba marejesho au anakuwa na mgonjwa ambaye anahitaji kumpeleka hospiutali kwa ajili ya kutibiwa kujengwa kw asoko hilo litakuwa mkombozi kwa mkulima anaweza akahifadhi mazao yake ghalani.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.