Kamisaa Sumaye ataja sababu CCM kushinda uchaguzi ujao serikali za mitaa

Kamisaa wa CCM, Zephania Sumaye akizungumza na wanachama wa chama chake katika Ukumbi wa Mikutano wa Mkoa wa Kilimanjaro mnamo Julai 18, 2024. (Picha na KISENA).

CCM MKOA, KILIMANJARO

Kamisaa wa Chama cha Mapinduzi (CCM), na Mkuu wa Wilaya ya Moshi Zephaniah Sumaye, amesema sababu za CCM kushinda Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, ziko nyingi ikiwemo ile ya wana CCM wenyewe kuvunja makundi ndani ya chama na kuwa wamoja.

Sumaye ameyasema hayo Julai 18, 2024 wakati alipopata nafasi ya kuwasalimia Viongozi wa CCM na Jumuiya   zake mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa CCM mkoani humo.

Amesema utaratibu wa kuvunja makundi ndani ya chama umeleta tija, jambo ambalo limeleta umoja na mshikamano ndani ya wanachama hao.

Silaha nyingine ya ushindi ndani ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni moyo wa dhati wa wanachama wa kujitolea katika shughuli mbalimbali za maendeleo zinazofanyika ndani ya kata zao.

Kwa upande wake Kamisaa wa Chama cha Mapinduzi na Mkuu wa Wilaya ya Hai, Amir Mkalipa, amesema Ibara ya 14 kifungu cha 3 cha Katiba ya CCM Kila mwana chama anahaki ya kuchagua na kuchaguliwa

“ili uweze kushika dola lazima apatikane mgombea anayetokana na CCM, na CCM ndio chama chenye hazina kubwa ya viongozi ambao wanaweza kuongoza dola.”amesema.

Aidha amesema utofauti wa CCM na vyama vingine vya siasa ni kwamba CCM ndio chama pekee chenye mabalozi Afrika na duniani kote, ambao kazi yao kubwa ni kuratibu Wanachama wake kwenye eneo lake, balozi ndiye anayejua idadi ya wanachama wake lakini pia na wapinzania wake.”

Aidha Mkalipa, alimpongeza Mbunge wa Jimbo la Moshi mjini kwa kazi nzuri anayoifanya ya kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2020 mpaka 2025.







Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.