Mradi wa Kirua-Kahe kugharimu Mil. 500; Ruwasa yasema utakamilika Agosti 30, 2024

KIRUA-KAHE, MOSHI

Wakala ya Usambazaji Maji na Usafi na Mazingira Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Kilimanjaro, umesema mradi wa zaidi ya Sh milioni 500 unaotekelezwa Kata ya kirua Vunjo umefikia asilimia 80 na unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Agosti 30 mwaka huu.

Meneja wa RUWASA Mkoa wa Kilimanjaro Weransari Munisi, ameyasema hayo Julai 19,2024  wakati akizungumza kuhusu upatikanaji wa huduma ya maji katika kitongoji cha Kioa B kilichopo katika Kijiji cha Yamu Makaa kata ya kirua Vunjo Kusini.

Munisi amesema kukamilika kwa mradi huo uliozinduliwa na Mwenge wa Uhuru mwaka 2024 ni mwarobaini kwa Wakazi hao ambao kwa sasa wanapata maji kwa mgao mara tatu kwa sik

“Wananchi wa Kijiji cha Yamu Makaa hususani maeneo ya Pumu One, wanalalamika kwasababu uchache wa maji uliopo kutokana na ongezeko la watu , asilimia 50 ya maji ndio yale yanayopatikana maeneo hayo, na sisi tumeweka mgao katika maeneo hayo, mwanzo ilikuwa ni mara moja kwa wiki lakini kwa sasa tumeongeza mara mbili wananchi wanapata huduma ya maji

Ameongeza kuwa “Changamoto ya maji kijiji cha Yamu Makaa, linakwenda kuisha, Serikali inatekeleza mradi mkubwa maji wa zaidi ya Sh milioni 500, ambao kwa sasa umefikia takribani asilimia 80, kukamilika kwa mradi huu wa maji utakwenda kuwanufaisha wakaazi wapatao 6,959.”amesema Mhandisi Munisi.

Aidha Meneja huyo,  amekiagiza  Chombo cha Usimamizi wa Maji Kirua-Kahe, kusimamia kikamilifu mgao wa maji na kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma ya maji.

“Napenda kutoa maelekezo kwa chombo cha usimamizi wa huduma za maji Kirua-Kahe, kuhakikisha kwamba ratiba ya mgao wa maji, ambayo wameipanga kwa wananchi inazingatiwa kila eneo kulingana na siku yake kuisimamia kikamilifu,”amesema.

Juali 16 mwaka 2024 baadhi ya wananchi wa kijiji cha Yamu Makaa, ili walazimu kuandamana  wakiiomba Serikali kuwasaidia kukamilisha mradi huo ili waweze kuondokana na changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama wanayoipitia kwa sasa.

Kata ya Kirua-Vunjo Kusini ina jumla ya vijiji sita huku wakazi wapatao 27,495 wakitegemea mradi wa maji wa Kirua-Kahe ambao umekuwa hautoshelezi kutokana na idadi kubwa ya wakazi ukilinganisha na mahitaji.




Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.