Serikali yaipongeza TPC kutekeleza maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan


Halmashauri ya Wilaya ya Moshi Mkoani Kilimanjaro, imeupongeza uongozi wa Kiwanda cha Sukari cha TPC, kwa kuendelea kutekeleza maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kukaa na wadau wa maendeleo hususan wadau wa elimu kwa lengo la kuhamasisha kuunga mkoano juhudi za Serikali ya Awamu ya sita katika kuboresha miundombinu ya elimu sanjari na mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji hapa nchini.

Mwenyekiti wa Halmashuari ya Wilaya ya Moshi DC, Moris Makoi, ametoa pongezi hizo jana wakati akizungumza na Waanadishi wa habari ofisini kwake kuhusiana na mchango wa wadau wa maendeleo ndani ya halmashauri hiyo.

Makoi , aliupongeza uongozi wa kiwanda cha sukari TC kwa namna ambavyo kimeendelea kuiunga mkono Serikali ya Awamu ya Sita katika uboreshaji wa miundombinu ya elimu ya msingi na sekondari huku akisema kuwa uboreshaji huo wa miundombinu ya elimu, imewezesha idadi ya wanafunzi kuongezeka kutokana na maboresho yaliyofanyika katika shule hizo.

“Nawapongeza sana wadau wa maendeleo ndani ya halmashauri yetu, hususan uongozi wa Kiwanda hiki cha sukari TPC kupitia taasisi yake tanzu ya FTK, kwani wamekuwa ni watu muhimu katika kuboresha sekta ya elimu kwani  wamewezesha kuzikarabati shule za msingi na zilizokuwa chakavu.”alisema Makoi.

Aidha alisema kuwa Kiwanda cha Sukari TPC  kimeanzisha mpango maalumu wa kuziboresha shule za msingi zilizopo kwenye vijiji vinavyozunguka kiwanda hicho, mpango huo unahusisana  ujenzi wa majengo mapya na kufanya ukarabati mkubwa uliogharimu kiasi cha Sh milioni 200 huku shule ya msingi Kiyungi ukarabati wake ukigharimu kiasi cha Sh milioni 56.

“Sote tumeshuhudia namna ambavyo shule zilivyoboreshwa kwa kujengwa vyumba vya madarasa, maabara, maktaba, nyumba za walimu, vifaa vya kujifunzia na kufundishia, ujenzi wa matundu ya vyoo na mabweni, mimi kama Mwenyekiti wa Halmashuari ya Wilaya ya Moshi Vijijini, napenda kuupongeza sana uongozi wa kiwanda cha sukari TPC kwa namna ambavyo kimeendelea kuiunga mkono serikali ya awamu ya sita katika uboreshaji wa miundombinu ya elimu ndani ya wilaya yetu,”alisema.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa Kata ya Arusha Chini, Diwani wa Kata hiyo Leonard Waziri, alisema awali shule hizo zilijengwa tangu miaka 1936, zilikuwa na hali mbaya kutokana na uchakavu wa majengo yake huku majengo mengine kutaka kuanguka.

Kwa upande wake Afisa mtendaji Mkuu wa Kiwanda hicho anayeshughulikia masuala ya Utawala Jaffari Ally, alisema mkakati wa TPC ni kujenga mahusiano mazuri na jamii inayo wazunguka, halmashauri ya Wilaya ya Moshi pamoja na Serikali Kuu.

Alisema kuwa Kiwanda hicho sambamba na uzalishaji wa sukari ikimeweka mikakati mbalimbali ya kusaidia jamii inayowazunguka ikiwemo uboreshaji wa elimu kwa shule za awali, msingi na sekondari, lengo likiwa ni kuimarisha ujirani mwema.

“Hivi karibuni tumejenga shule mpya ya sekondari ya Chekereni Weruweru, kutokana na wanafunzi kutoka umbali mrefu wa kilometa 27 kuja kusoma shule ya sekondari TPC na kwamba shule hiyo imesaidia wanafunzi hao kwa sasa wanapata huduma bora ya elimu katika shule yenye mazingira bora na karibu.”

Aliongeza “Kiwanda cha TPC kupitia taasisi yake ya FTK inawafadhili wanafunzi 250, kusoma Vyuo vya Ufundi Stadi na Vyuo Vikuu kila mwaka bila kuchangia gharama zozote na bila masharti kwamba wakimaliza masomo yao wajekufanya kazi TPC,”.

Alisema wapo baadhi ya wanafunzi wanapoomba mikopo na hupewa pengine asilimia 60 na kiwanda huwajazilizia asilimia 40 inayobakia na wamekuwa wakiyafanya hayo wakiamini kwamba wanapoisaidia jamii wanalikomboa taiofa kiuchumi.

Aidha alisema asilimia kubwa ya bajeti TPC ni kwa ajili ya huduma za kijamii katika sekta ya afya, elimu, miradi mikubwa ya umwagiliaji pamoja na ujenzi wa majosho kwa ajilia kuwezesha mifugo ya wafugaji kupata huduma nzuri.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.