KALOLENI, MOSHI
Zaidi ya Sh bilioni 1.3 za miradi ya maendeleo zimepelekwa katika Kata ya Kaloleni iliyoko Halmashauri ya Manispaa ya Moshi na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.
Diwani wa Kata hiyo Nassib Mariki, ameyasema hayo Julai 22,2024 wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo, kwenye mkutano wa hadhara wa wananchi wa kata hiyo, mkutano uliofanyika katika uwanja wa Ofisi ya diwani huo.
Amesema katika kipindi cha miaka mitatu na nusu, Serikali imepeleka fedha nyingi za utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo miradi ya Afya, Elimu, Barabara, Kilimo, fedha kwa ajili ya mikopo pamoja na ukarabati wa kituo cha polisi.
Amesema kutokana na changamoto ya idadi kubwa ya wanafunzi shule ya seokondari Msasani, Serikali kuu katika mwaka wa fedha 2023/2024, imewapatia kiasi cha Sh milioni 584.2 kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya ya sekondari katika kata hiyo.
Akizungumzia mikopo ya akina Mama, Vijana na watu wenye ulemavu, kwa kipindi cha uongozi wake jumla fedha ambazo zimepelekwa kwenye jamii ni Sh milioni 164. 2 25, 627.
Kwenye Sekta ya Kilimo Mariki amesema jumla ya Sh milioni 225,160,000 zimetumika katika ununuzi wa mashine ya kukoboa mpunga, ukamilishaji wa miundombinu ya choo cha ofisi pamoja na mbolea ya ruzuku.
Aidha maesema kwenye sekta ya afya diwani huyo amesema jumla ya Sh milioni 22, 700,000 zimetumika katika ununuzi wa jokofu la kuhifadhia dawa za chanjo, ukarabati wa jongo la zahanati pamoja na darila zahanati hiyo.