Muwsa yakamilisha mradi wa uboreshaji wa huduma ya maji Old Moshi Mshariki

OLD MOSHI MASHARIKI, MOSHI

Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Moshi Mjini (MUWSA), imekamilisha mradi wa uboreshaji wa huduma ya Maji Safi na Salama uliokuwa ukitekelezwa katika Kata ya  Old Moshi Mashariki kwa kulaza mambomba ya maji kilo meta 39.9.

Kaimu Ofisa  Mawasiliano wa (MUWSA), Heavenlight Mariki, aliyasema hayo, wakati akizungumza kwenye mkutano wa Serikali ya Kijiji cha Tsuduni, ulioketi kwa ajili ya kuzungumzia changamoto ya upatikanaji wa maji katika kijiji hicho.

Alisema katika mradi wa uboreshaji wa huduma ya maji Kata ya Old Moshi Mashariki, Mamlaka hiyo, imetumia kiasi cha Sh milioni 843, kwa kulaza mabomba ya maji, umbali wa kilometa 39.9 ambapo kwa sasa wananchi watatakiwa kuhamishwa kutoka kwenye  miundombinu ya maji ya zamani kwenda kwenye mambo mapya kwa ajili ya kuanza kufungiwa mita za maji.

Alisema mteja mwenye bomba lake nyumbani, fundi atakuja kulikagua bomba hilo kama lina kidhi vigezo atahamishiwa kwenye laini  mpya na kuendelea kupata huduma huku ukiwa umefungiwa mita na kwa mteja ambaye hana bomba la maji nyumbani atafanyiwa upembuzi yakinifu, ambapo atatumiwa gharama zake kwa kujaziwa fomu na kulipa gharama hizo MUWSA itakuja na kumfungia huduma hiyo ya maji.

Aidha Mariki aliwataka wananchi kuvitunza vyanzo vya maji pamoja na miundombinu hiyo ya maji, huku akionya kuwa ni marufuku mteja yeyote kujiunganishia maji, kwani kwa kufanya hiyo ni kuhujumu miundombinu hiyo na sheria kali zitachukuliwa didi yake.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.