MBUNGE wa Jimbo la Mwanga Joseph Tadayo, amekagua ujenzi mpya wa shule ya sekondari Toloha na kuweka jiwe la msingi kwenye shule hiyo.
Toloha ni miongoni mwa shule za kata ambazo zilikuwa hazina kabisha shule ya sekondari na kulazimika watoto kutembea umbali mrefu kwenda kata ya jirani kufuata elimu.
Akizungumza na Wakazibwa kata hiyo iliyopo kwenye halmashauri ya Mwanga, Tadayo alisema ujenzinwa shule hiyo ni utekelezaji wa maamuzi ya serikali ya awamu ya sita baada ya kubaini kuwa watoto wengi hususani wa kike huwafanyia vizuri kwenye masomo yao.
"Leo tulikuja hapa kata ya toloha, kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa shule ya sekondari, kata hii ndio ilikuwa ya mwisho iliyokuwa imebakia katika jimbo la mwanga kuwa na shule ya sekondari."
Alisema wanafunzi tayari wako madarasani na shule kwa ujumla.imemalizika kwa asilimia 99%, ina madarasa ya kutosha yenye viwango cha juu,.
"Tunamshukuru sana Rais Samia kwa uamuzi wake wa kutujengea shule hii hapa imeondoa adha ya wanafunzi kutembea umbali mrefu kufuata elimu maeneo mengine,".
Akitoa taarifa ya ujenzi wa mradi wa huo Afisa Elimu Sekondari R Mnzava, alisema walipokea Sh bilioni 5.8 kutoka serikali kuu kwa ajili ya ujenzi wa shuke hiyo chini ya mradi wa Sequit.
"Utekelezaji wa mradi huu ulihusisha ujenzi wa vyumba vya madarasa nane, jengo la utawala, jengo la tehama, maabara za masomo ya sayansi, chemistry, biology na physics pamoja na matundu ya vyoo nane." Amesema.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji cha Kalambandea Papaa King Laizer, ameishukuru Serikali kwa kuwajengea shule katika kata hiyo.
Amesema changamoto iliyopo kwa sasa ni tembo ni wengi ameomba serikali kuiongezea fedha shule hiyo kwa ajili ya kujenga mabweni mawili, ili wanafunzi waweze kulala shuleni hapo.
Nao baadhi ya wakati wa kata hiyo Mwajabu Ally Mkilindi na Rebeca Richard, tunafuraha kubwa sana ya kujengewa shule hapa, imewaondolea watoto wetu kutembea umbali mrefu kwenda kata ya Kwakoa, Kigonigoni na Kwangu.

.jpg)




