MWANGA, KILIMANJARO
Mbunge wa Mwanga Joseph Tadayo, amewataka wanafunzi kuwa na nidhamu na kutojihusisha na vitendo viovu vitakavyowasababisha kufukuzwa shule, huku pia akiwataka kuongeza jitihada kwenye masomo yao darasani.
Akizungumza na wakazi wa kata ya Kivisini, Tadayo amesema kumekuwa na utovu wa nidhamu kwa wanafunzi hatua ambayo imewafanya wengine kufukuzwa shule na kuleta usumbufu kwa wazazi na walezi wao.
Aidha Tadayo amesema fedha zilizopelekwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo ikiwamo sekta ya elimu ni nyingi huku akiweka bayana Shule ya Sekondari Kivisini ikipokea kiasi cha Tshs. Mil. 479
"Ujenzi wa shule ya sekondari Kivisini Tsh ml 479 kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne. Ujenzi kidato cha tano na sita katika shule hiyo uliohusisha madarasa sita, mabweni mawili, na matundu ya vyoo 10 kwa Tsh milioni 429. Ujenzi wa nyumba za walimu sekondari kwa Sh milioni 98 na ujenzi wa zahanati Tsh milioni 50; Ujenzi wa nyumba ya watumishi wa Afya Tsh milioni 50," amesema Tadayo.
Kwa upande wake Afisa Elimu Sekondari wilaya ya Mwanga Rubeni Mzava amesema zaidi ya shilingi milioni 300 zimetumika katika ujenzi wa madarasa sita, na matundu ya vyoo
"Tunaishukuru sana serikali kwa kuweza kukamilisha miradi hii, Kwa sasa kata zote zina shule.za sekondari , hizi zote tunatambua kazi zako kubwa na haya yote ni matunda ya kazi za Mbunge Tadayo. Sisi.sote tunafurahia uwepo wa.shule hii katika kata ya Kivisini, leo umetembelea majengo haya yanayojengwa ya kidato cha tano na sita ambapo kuna madarasa sita yaliyojengwa na kugharimu sh milioni 150, Ujenzi wa mabweni mawili yenye uwezo kwa kila mmoja kuchukua wanafunzi 80, yaliyogharimu sh milioni 160, vyoo vyenye matundu 10 yaliyogharimu Sh milioni 19.
