MAWENZI, MOSHI
Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Mawenzi, iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, inatarajia kuanza rasmi huduma ya kusafisha figo kwa wagonjwa wanaofika hospitalini hapo, ili kukabiliana na wimbi la kuongezeka kwa wagonjwa wanaohitaji huduma hiyo.
Hayo yamebainbishwa Julai 15,2024 na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mawenzi (MRRH) Dkt. Edna-Joy Munisi, wakati uzinduzi wa Wodi ya upasuaji ya Wanaume iliyopo katika taasisi hiyo.
“Siku ya leo tumepata ugeni wa Mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini Priscus Tarimo, ambapo amekuja kwa ajili ya uzinduzi wa gari la Wagonjwa, pamooja na kuzindua ukarabati wa wodi ya upasuaji ya wanaume, pamoja na kukagua maendeleo ya ukarabati wa wodi ambayo itakwenda kutumika kwa ajili ya kutoa huduma za kusafisha figo, “ alisema Dkt. Munisi.
Dkt. Munisi amesema Serikalai imetenga kiasi cha Sh milioni 342, ambazo zitatumika katika ujenzi unaoendelea wa miundombinu itakayokuwa mwenyeji wa idara ya huduma ya kusafisha damu, ambazo zinatarajiwa kutumika kwa ajili ya kukarabati,
Akizungumzia gharama za kusafisha figo, Dkt. Munis alisema gharama hizo zitatolewa kulingana na muongozo unavyowataka huku akiishukuru Serikali kwa kuweka utaratibu mzuri ambao unawawezesha wananchi wote kuwa na Bima ya afya kwa wote.
“Tunatarajia siku za hivi karibuni kuanza kutoa huduma za kusafisha figo, baada ya ukarabati huu kukamilika, tutaweza kuwa na huduma ya kusafisha figo katika hospitali yetu ambapo jumla ya vitanda 10 pamoja na mshine zake zitakwenda kutoa huduma kwa wakati mmoja,”alisema.
Aidha alisema wagonjwa wa upasuaji wameongezeka kutokana na ajali, huku akisema kuwa wahanga wakubwa wanaopokelewa katika hospitali hiyo ni wale wa ajili za pikipiki, ali maarufu (Bodaboda) hawa wamekuwa ni sehemu kubwa ya wagonjwa wanaowahudumian katika hospitali hiyo.
