Figo ni moja ya viungo muhimu vya mwili wa binadamu na kazi yake kuu ni kuondoa taka kutoka mwilini kwa njia ya mkojo.
Figo hutenganisha vitu kutoka kwenye damu, ambavyo ni hatari kwa mwili wa binadamu, ikiwa ni pamoja na baadhi ya madini yasiyo ya lazima, na kisha damu safi huzunguka katika mwili.
Kwa mujibu wa Dkt. Milli Mathew, ambaye ni Mkuu wa Hospitali ya MGM Health Care anasema, kadiri ugonjwa wa figo unavyoendelea, dalili hizo huonekana na unaweza kuelewa maendeleo haya kupitia uchunguzi na vipimo vya afya pekee.
Anasema ugonjwa wa figo hudumu kwa muda mrefu na mara nyingi huwapata watu wenye kisukari au watui wemnye shinikizo la damu.
Anasema watu wanaougua ugonjwa huo hupata shida kupata haja ndogo au kuwa na damu kwenye mkojo.
Kwa mujibu wa tafiti zilizofanyika hivi karibuni na Shirika la India la Nephrology, zinaonesha kuwa watu milioni 84 duniani kote, wanaugua magonjwa mbalimbali ya figo, ambapo mtu mmoja kati ya watu kumi duniani ana aina fulani ya ugonjwa wa figo.
Ikumbukwe kwamba kati ya sababu kumi za vifo duniani, ugonjwa wa figo unatajwa kushika nafasi ya saba.




