Wananchi Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro, wameaaswa kuchangia huduma ya maji inayopatikana katika maeneo yao na kwamba fedha hizo wanazochangia zinasaidia katika kuboresha upatikanaji wa huduma hiyo kwenye maeneo husika.
Mratibu wa Vyombo Vya Watoa Huduma ya Maji Ngazi ya Jamii kutoka Ofisi ya Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA), Wilaya ya Same Anastazia Isaya, ametoa wito huo kwenye kikao cha wadau wa maji wakiwamo wenyeviti wa Vijiji, Kata, Madiwani pamoja na Viongozi wa Jumuiya za Watumia Maji Ngazi ya Jamii (CBWSO) kutoka Kata zote zinazohudumiwa na vyombo hivyo vilivyoko Jimbo la Same Mashariki.
Isaya amesema kuwa Serikali imekuwa ikitumia gharama kubwa katika kuwapelekea wananchi wake huduma ya Maji Safi na Salama hapa nchini, ili waondokane na matumizi ya maji yasiyo salama kwa afya zao.
Aidha amewataka wananchi Wilayani humo, kuipa kipaumbele huduma ya maji kutokana na umuhimu wake katika maisha ya mwanadamu huku akibainisha changamoto zilizopelekea miradi mingi ya maji ya zamani iliyokuwa ikishikiriwa na Kamati za Maji (COWSO) kushindwa kujiendesha kutokana na kukosa fedha za matengenezo ya miradi hiyo.
Wakizungumza katika kikao hicho, baadhi ya Wenyeviti wa Vijij, walibainisha changamoito ambazo zinapelekea wananchi kushindwa kuchangia huduma ya maj, ikiwemo ubovu wa miundombinu ya maji ya zamani inayosababishwa na upotevu mkubwa wa maji njiani.
Aidha walisema wananchi wako tayari kuchangia huduma ya maji na kuutaka uongozi wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingi Vijijini (RUWASA), kuirekebisha miundombinu ya bomba za maji za zamani.
Katika hatua nyingine Viongozi hao waliipongeza Serikali kwa kuja na utaratibu wa kuchangia huduma ya maji kwa kutumia mfumo wa Serikali wa GEPG, ambao umesaidi kuweko kwa uaminifu wa fedha zao pindi wanapochangia tofauti na huko nyuma ambapo fedha hizo zilikuwa zinaishia mikononi mwa wajanja na kupelekea miradi mingi ya maji kufa.
Nao baadhi ya wakazi wa kijiji cha Ndungu Rehema Senzi na mkazi wa kijiji cha Msufini Omari Mganga, walisema hali ya upatikanaji wa maji bado ni changamoto kubwa katika maeneo yao ambapo wanalazimika kupata maji ya bomba kwa wiki mara mbili.
Kwa upande wake diwani wa Kata ya ndungu Abeid Salehe na diwani wa kata ya kihurio MarianeAabraham, walisema miradi ya maji iliyokuwepo hapo awali ilichangiwa kufa na baadhi ya Viongozi wa Kamati za COWSO kwa kushindwa kutoa taarifa za mapato na matumizi ya makusanyo ya fedha za maji hali iliyopelekea wananchi kugoma kuchangia