Mbunge Mstaafu Moshi Mjini atoa msaada Gereza la Karanga Moshi

Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Moshi Mjini Jafari Michael, ametoa msaada wa vyakula kwa wafungwa na mahabusu wa Gereza Kuu la Karanga lililopo Moshi, mkoani Kilimanjaro, kama sehemu ya kusheherekea Sikukuu ya Eid el Adh’haa inyotarajiwa kufanyika Juni 17 mwaka huu.

Akikabidhi vitu hivyo mnamo Juni 15,2024 kwa niaba ya Mbunge Jafari, Katibu wake Deogratius Kiwelu, amesema imekuwa kawaida yake mbunge huyo wa zamani, kutoa misaada hiyo ya kibinadamu kwa ajili ya kuisaidia jamii yenye uhitaji wakiwemo watoto yatima, wazee, wafungwa na mahabusu ambao wengine hujikuta wakikosa msaada kutokana na nduzu zao kuishi mbali, kama sehemu ya sadaka yake.

“Kwa niaba ya aliyewahi kuwa mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini Jafari Michael, nimekabiddhi mafuta ya kula lita 40 na mchele kilo 250, kwa ajili ya wafungwa na mahabusu wa gereza la Karanga, ambao wataungana na waumini wengine wa dini ya Kiislamu kusheherekea Sikukuu ya Eid el Adh’haa inyotarajiwa kufanyika Jumatatu ya Juni 17 mwaka huu”, amesema.

Aidha Kiwelu ametoa wito kwa wadau wengine kujitokeza kuwasaidia wahitaji mbalimbali  katika jamii ili kuwawezesha kukabiliana na changamoto wanazozipitia katika wakati huo.

Kwa mujibu wa uongozi wa gereza hilo, umemshukuru Mbunge mstaafu Jafari Michael, kwa msaada huo na kuelezea kuwa utawasaidia wafungwa na mahabusu hao, kusheherekea pamoja na waumini wengine katika Sikukuu ya Eid el Adh’haa.

Baraza Kuu la Waislamu Tanzanaia (BAKWATA) limesema Sikukuu ya Eidel itafanyika Juni 17 mwaka 2024  na suala yake itaswaliwa katika Msikiti wa Mohamed VI uliopo Makao Makuu ya Baraza hilo Kinondoni.





Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.