Umoja wa Machifu Kilimanjaro wapongeza Rais Samia kutunukiwa Honoris Causa

Umoja wa Machifu Mkoa wa Kilimanjaro umesema juhudi kubwa za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuboresha mahusiano kati ya Tanzania na nchi zingine duniani ni hatua kubwa ambayo itaijenga Tanzania kiuchumi.
 

Mwenyekiti wa Machifu Mkoa wa Kilimanjaro Frank Marealle ameyasema hayo Juni 8,2024 wakati akitoa salamu za umoja huo za kumpongeza Rais  Samia kwa kutunukiwa Shahada ya Udaktari wa Falsafa ya Heshima (Honoris Causa) ya Chuo Kikuu cha Sayansi ya Anga cha Korea Kusini, hivi karibuni.

 

Chifu Marealle amesema ziara ya Rais Samia nchini Korea na mikataba ambayo nchi ya Tanzania imeingia na Korea ni udhibitisho wa wazi jinsi Dkt. Samia anavyoendeleza kwa umakini Sera ya Taifa ya Mambo ya nje ya mwaka 1964/1965 na maboresho yake ya mwaka wa 2001.

 

Akizungumzia tuzo hiyo ambayo umoja huo unampongeza Rais Samia kwa kuipata, Chifu Marealle amesema  kuwa ni heshima kubwa kwa Rais na Tanzania kwa ujumla ikiwa ni ‘tuzo’ kwa Rais na Taifa kwa kazi kubwa ambayo imefanywa kwa kuboresha huduma za anga hapa nchini.

 

Amesema marekebisho mengine yanayohusiana na usafiri wa anga hapa nchini pia yamechangia Rais Samia kupata tuzo hiyo kutokana na ukweli kuwa marekebisho hayo yatachangia kwa kiasi kikubwa kukua kwa uchumi wa Taifa.

 

Aidha ametoa wito kwa Watanzania kuendelea kuiamini serikali inayoongozwa na Rais Samia pamoja na kumuunga mkono ili Taifa liendelea kuwa imara zaidi na hivyo kuwavutia wawekezaji wengi zaidi jambo ambalo litakuza uchumi wa Taifa na ule wa wananchi wote kwa ujumla.

 

Chifu Amani Mapombe, kutoka   Tarafa ya Mwembe-Mmbaga Wilaya ya Same, amesema mkoa wa Kilimanjaro unayo mazao mbalimbali yanayozaliwshwa na wananchi yakiwemo maparachichi, ndizi, tangawizi, pilipili, na ziko fursa nyingi za kiuchumi katika mkoa wa Kilimanjaro mkoa wa Kilimanjaro na Arusha na kuiomba Serikali kujenga viwanda  viwanda ambavyo vitakuwa vikiyachaakata mazao hao na kuasindika.

Naye Chifu wa Siha Godfrey Kileo, amempongeza Rais Samia kwa ziara yake Korea Kusini. Ziara abayo imeugusa mkoa wa Kilimanjaro moja kwa moja, ikiwemo ujenzi wa kiwanja cha ndege Moshi.

Amesema Mkoa wa Kilimanjaro, Tanga na Arusha ni mikoa ambayo inazalisha mazao mengi yenye masoko makubwa duniani wanaamini kwa ziara hiyo itaongeza uwezo mkubwa kwa serikali kuweza kuwasaidia wananchi kufikisha mazao katika masoko ya nje na kuongeza uchumi.

Katibu wa Baraza la wazee mkoa wa Kilimanjaro, Godson Lucas, amesema shahada ya udaktari wa anga aliyoipata Rais samia  imeiletea heshima kubwa nchi ya Tanzania na Africa nzima, kwani imeonyesha namna gani Rais anavyoheshimika katika mataifa.








 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.