Visima vinavyotumika na Zimamoto na Uokoaji Kilimanjaro kutambuliwa kisheria

MAJENGO, MOSHI

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu, ametoa maelekezo.kwa Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, kuhakikisha kwamba maeneo yote yenye visima vya kuchotea maji yanayotumika kuzima moto yanatambuliwa kisheria na kuwekewa vibao.

 Maagizo hayo aliyatoa wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa gari jipya la Zimamoto na Uokoaji, lilolotolewa na serikali mkoani humo kwa ajili ya kukabioiana na majanga ya moto.

 Babu aliutaka uongozi wa Manispaa hiyo, kuhakikisha kwamba maeneo yote ambayo yana visima vya kuchotea maji yalijengwa na Wakoloni, yanaimarishwa na kuwekewa vibao ambavyo vitaonesha kuweko na bomba la kuchotea maji ya kuzima moto.

Mkurugenzi hakikisha maeneo yote yenye visima vya kuchotea maji ya kuzima moto yanahuishwa na wananchi wasiendelee kuyachezea, nimefahamishwa hapa kuwa kuna visima takribani 142 hakikisheni mnavijengea vibao vitakavyoonesha kuwa kuna bomba la maji hapo", alisema.

Katika hatua nyingine mkuu huyo wa mkoa amekipongeza kiwanda cha sukari TPC kwa utayari wao wa kutoa gari la Zimamoto kuja kusaidia majanga ya moto pale yalipokuwa yakitoea.

Kutoka TPC hadi Moshi mjini ni zaidi ya kilometa 17, lakini mliweza kutuma magari yenu na kuja kusaidia uokoaji, kwa kweli mmekuwa msaada mkubwa sana kwa wananchi wa Manispaa ya Moshi.

“Mtakumbuka kuna janga la.moto lililotokea na kuunguza vibanda vyote vya soko la Mbuyuni, ilikuwa saa saba na dakika tano usiku, niliwapigia simu usiku huo na wakaweza kufika kwa wakati na kusaidia kuzima moto huo,” aliongeza Mkuu wa Mkoa





 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.