SHANTY, MOSHI
Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na wadau wa Maendeleo likiwemo Shirika la Kilimo na Chakula Duniani (FAO) na Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU) wamekubaliana kuweka mikakati ya pamoja ya kupanua wigo wa masoko ya mazao kwenda nchi za nje.
Meneja uzingatiaji wa Afya ya Mimea na Mamlaka ya Afya na Viatilifu vya Mimea Tanzania (TPHPA) Mdili Katemani, aliyasema hayo jana, wakati wa warsha yenye lengo la kuongeza upatikanaji wa masoko ya mazao ya Kilimo yanayozalishwa Tanzania, warsha iliyofanyika Mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro.
Alisema Mradi wa STREPHIT ambao unafadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) na Shirika la Kilimo na Chakula Duniani (FAO) wana mkakati wa kufungua masoko mapya ya mazao mengine matano huku wakilenga kuzifikia nchi 15.
“FAO na EU wanatekeleza mchakato huo kupitia Mradi wa Kuimarisha huduma za Afya ya Mimea kwa Usalama wa Chakula Tanzania (STREPHIT), kama mnavyofahamu hivi karibuni tumeanza kufungua masoko ya mazao kama vile Parachichi, mashudu ya pamba, lakini katika mwendelezo huo, kupitia mradi wa STREPHIT, unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya, pamoja na Shirika la Kilimo na Chakula Duniani (FAO) sasa hivi tuna mkakati wa kufungua tena masoko mengine mapya matano ya mazao, ambapo tunalenga katika nchi 15 kuweza kufikisha mazao hayo.
Aliyataja mazao hayo kuwa ni pamoja na nanasi, pilipili manga, karafuu, kokoa na vanila, mazo ambayo tumeyawekea mkakati kwa sasa ili tuweza kuyafikisha sehemu nyingine duniani ambako tulikuwa hatuyapeleki.
“Utaratibu wa Kimataifa, unataka ili uweze kufikia soko jipya ni lazima kwanza uandae orodha ya Kitaifa ya visumbufu vilivyoko nchini kwako, ambavyo vina athiri zao hilo, halafu baada ya kuandaa orodha hiyo tunatakiwa tuandae nyaraka ambayo itakuwa inaeleza kwa undani kuhusu uzalishaji wa zao husika unavyofanyika hapa nchini na taarifa hizo tunapaswa kuziwasilisha kwenye nchi ambazo tunazilenga”,alisema Katemani.
Aliongeza kuwa endapo
watafanikiwa mpango huo wanalenga soko
lenye ukubwa wa Dola za Marekani bilioni 3.1 katika mazao hayo matano
wanayotarajia kuyasafirisha kwenda nje.
“Lengo la serikali ni kuhakikisha kuwa masoko mengi yanapatikana kutokana na ukuaji wa sekta ya Kilimo nchini, katika warsha hii elimu pia itatolewa kwa washiriki wake jinsi ya kuandaa jarida la upatikanaji wa soko litakalosaidia kufua masoko mapya ya nje na hivyo kuongeaz pato la taifa”,alisema.
Kwa upande wake Afisa Biashara kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara Andrea Assenga, alisema warsha hiyo ni muhimu kutokana na lengo lake ambalo alisema lilikuwa na lengo la kuhakikisha wakulima wanapata masoko mapya mazuri nay a uhakika ya biadhaa zao.
“Serikali kupoitia Wizara zake ya Boiashara na Viwanda ityaendelea kuhakikisha wakulima wanapata elimu itakayowawezesha kuzalisha bidhaa nyingi na zernye ubora, hatua ambayo itasaidia kupata masoko mengi na kudumisha soko la zamani la mazao ya kilimo Tanzania,”
Naye Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzanaia (TFRA) Gothard Limpawe alisema mbolea inaunganishwa moja kwa moja na mipango ya afya ya mimea linapokuja suala la kuongeza uzalishaji wa chakula nchini.
“Jukumu letu la msingi ni kuhakikisha mbolea inayoingizwa nchini au inayozalishwa nchini inakuwa nzuri , leno ni kuhakikisha mbegu bora inazalishwa na hivyo kuzalisha mazao bora yatakayoliwezesha taifa kupata masoko mengi nje ya nchi na hivyo kuongeza uzalishaji wa mbegu bora.”alisema.