
Diwani wa Kata ya Korongoni Heavenlight Kiondo
KORONGONI, MOSHI
Diwani wa Kata ya Korongoni, Halmashauri ya Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro HeavenLight Kiondo, amesema kuwa mikopo ya asilimia 10% inayotarajiwa kutolewa na Serikali itawasaidia wanawake wajasiriamali, vijana na watu wenye ulemavu kujikwamua kiuchumi.
Kiyondo amesema.hayo Mei 18, 2024 wakati akizungumzia changamoto mbal8mbali zinazowakabili wananchi wa kata yake na kuzitafutia ufumbuzi.
Amesema urejeshwaji wa mikopo ya asilimia 10% ambayo hutolewa na Serikali kupitia halmashauri bila riba, itawasaidia wanawake Wajasiriamali, vijana na wenye ulemavu kujikwamua kiuchumi kwa.kubuni fursa mbalimbali za kiuchumi , huku akimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa.kuruhusu mikopo hiyo kurejeshwa tena baada ya kusitishwa.
Naoa baadhi ya wakazi wa kata hiyo, Neema Nkungu na Faima Rasuli, wamemshukuru diwani huyo kwa.ziara yake ya mtaa.kwa mtaa , ambayo ameianzisha kwa.ajili ya kutytua kero zinazowakabili wananchi katika mitaa yao ili kuzipatia changamoto hizo ufumbuzi wa akudumu.