Chama cha soka mkoani Kilimanjaro (KRFA), kinatarajia kufanya kikao chake Mei 18, 2024 , kitakachokuwa na lengo la kujadili mambo mbalimbali yanayohusu ligi ya wanawake msimu huu.
Taarifa hiyo imetolewa na Katibu wa chama cha soka mkoani humo Harold Kifunda, kwa waandishi wa habari juu ya maandalizi ya kikao hicho ambapo kikao hicho kinatarajia kushirikisha kamati ya soka mkoa wa Kilimanjaro, kamati ya mashindano KRFA , kamati ya waamuzi , kamati ya ufundi na uongozi wote wa vilabu vya soka la wanawake mkono humo, na vituo vinavyo miliki timu za wanawake mkoani Kilimanjaro.
Aidha maesema mkutano huo unatarajiwa kuwa na agenda mbili.ambazo ni kujadili ligi ya wanawke na hali ya soka la wanawake ilivyo mkoani humo.
Mnamo Januari 29, 2024 KRFA ilifanya mkutano mkuu katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (Ushirika Conference Center-UCC) ambapo Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Kilimanjaro Isaac Munis alisema soka la Wanawake mkoa wa Kilimanjaro bado liko nyuma sana na kuziomba Kamati ya soko la Wanawake na Vijana kuongeza bidii kuendelea kuwekeza nguvu zaidi katika timu za mpira wa miguu kwa Wanawake kwenye Wilaya huku akitoa maagizo kwa viongozi wa Vyama vya soka vya Wilaya kuhakikisha chaguzi kuanzia ngazi za chini zinafanyika kupata safu bora ya uongozi utakaorejesha heshima ya KRFA.
Katika hotuba yake Mwenyekiti alijikita zaidi kwenye maendeleo ya mpira wa miguu kwa ujumla, ambapo ameviasa Vyama vya Mpira vya Wilaya (FA) kuongeza bidii ili kuleta maendeleo ya mpira wa miguu kwenye wilaya hizo kwa kuwatumia zaidi wachezaji vijana wenye umri chini ya miaka ishirini (U20) ili kusaidia kuibua, kuvitengeza, kuvikuza na kuviendeleza vipaji vya vijana hao.
Alisisitiza kuwa KRFA imeendelea na mikakati ya kupandisha timu kila mwaka, ambapo mwaka 2022 imepandisha TRA na mwaka 2023 ilipandisha tuimu ya Tanesco ambapo amesema malengo ifikapo mwaka 2026/27 KRFA kuwa na timu inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania.
Aidha amesema chama hicho kimepiga hatua kubwa katika kuzalisha vijana wenye vipawa vya kucheza timu mbalimbali zilizoko katika ligi kuu Tanzania lakini pia hata kwa viongozi walioko katika Chama Cha Soka Mkoa wa Kilimanjaro.
Kwenye suala la waamuzi mkoa Mwenyekiti huyo, amesema mkoa huo haukuwahi kuwa na mkufunzi wa waamuzi, kwa kipindi cha uongozi wake wamefanikiwa kumpata Godbles Kimaro, ambaye kwa sasa ndiye Mkufunzi wa Waamuzi mkoani humo.
