Sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa, sura ya 290 ilifanyiwa marekebisho mwaka 2018 ili kuweka masharti kwa Halmashauri zote nchini kutenga fedha kwa ajili ya mikopo kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.
Diwani wa Kata ya Korongoni Heavenlight Kiyondo
Kanuni ya 4 ya Utengaji wa Fedha za Mikopo inamweka bayana Halmashauri inatakuwa na wajibu wa kutenga asilimia 10 ya Mapato yanayotoka katika vyanzo vyake vya ndani kwa ajili ya kutoa mikopo kwa vikundi vya wanawake asilimia 4, vijana asilimia 4, na watu wenye ulemavu asilimia 2.
Mnamo Aprili 13,2023 katika Bunge la 12 Waziri Mkuu wa Jamhuri Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa alitangaza usitishwaji wa mikopo hiyo ili kupisha utaratibu mwingine wa utoaji wa mikopo.
Baada ya mwaka mmoja, mnamo Aprili 16, 2024 Waziri wa TAMISEMI Mohammed Mchengerwa alitangaza kurejesha kwa mikopo hiyo wakati akisoma bajeti yake ya mwaka 2024/25.
Jumatatu ya Mei 13, 2024 Naibu Waziri TAMISEMI Zainab Katimba wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum Josephine Gezabuke aliwaondoa hofu wanawake, vijana na watu wenye ulemavu na kwamba mikopo hiyo rasmi itaanza kutolewa Julai Moshi 2024.
Katimba alisema Rais Samia Suluhu Hassan ameridhia kutolewa tena mikopo hiyo, bayana sababu iliyofanya isitishwe kuwa marejesho kwa vikundi vilivyokuwa vikidaiwa yalikuwa yanaendelea.
Shilingi bilioni 227.96 zinatarajiwa kutolewa kwa vikundi hivyo nchi nzima huku shilingi bilioni 63.67 zikiwa ni fedha za marejesho kwa mikopo ilitotolewa kabla ya kusimamishwa.
Hatua yetu inaanza katika kata ya Korongoni iliyopo Manispaa ya Moshi kwa Wanawake waliofaidika na mikopo ya Halmashauri.
Pia tumezungumza na Diwani wa Kata hiyo HeavenLight Kiyondo miongoni mwa wanawake viongozi katika Baraza la Madiwani Manispaa ya Moshi ambao Kata yake imefurahia mikopo hiyo kurejeshwa.
Mbali na mikopo hiyo Diwani Kiondo amewataka wanawake wenye watoto kutojisahau na malezi ya watoto wao ili mikopo hiyo iwe na maana, isitumike kama msumari katika kidonda.