Bingwa Zuberi Cup Tournament 2024 kujinyakulia Kombe na Sh. Mil. 3/-

Mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini Priscus Tarimo, ametangaza zawadi kwa mshindi wa Zuberi Cup Tournament 2024 kuwa atajinyakulia kitita cha Sh milioni tatu, mshindi wa pili akiweka kibindoni Sh milioni mbili na mshindi wa tatu akipata kiasi cha Sh milioni moja.

Tarimo alitangaza zawadi hizo mnamo Mei 18, 2024 kwenye uzinduzi wa mchakato wa kuanza kwa mashindano hayo yanayofadhiliwa na Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi Mhandisi Zuberi Kidumo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Soka mkoa wa Kilimanjaro Isaack Munis kwa jina maarufu Gaga, amesema kikwazo kikubwa cha maendeleo ya soko mkoani humo ni ubovu wa miundombinu ya viwanja, upungufu wa wataalamu wa tiba, na uhaba wa walimu wenye ueledi  wa kisasa.

Aidha Mwenyekiti wa Soka mkoani humo Munisi amesema wanajivunia mafanikio makubwa ya timu za mkoa wa Kilimanjaro licha ya kushindwa kuendelea mbele.

“Mshindano ya msimu huu mshindi ataondoka na Kombe na fedha taslimu Sh milioni tatu, mshindi wa pili atachukua Sh milioni mbili huku mshindi wa tatu atajinyakulia kitita cha Sh milioni moja”,.

Akizungumza Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi Mhandisi Zuberi Kidumo amezitakia kila la Kheri  timu shiriki katika maandalizi huku akisisitiza kuwa nidhamu ili kuufanya mchezo wa soka kuishi katika hadhi yake.

Naye mwakilishi wa vilabu vya mpira wa miguu mkoa wa Kilimanjaro Haman Gao aliwasilisha changamoto kwa Mbunge juu ya viwanja vya mpira vinavyo milikiwa na taasisi kuwa vigumu kutumiwa na vilabu vya mkoa huo na kumuomba Mbunge kuiwasilisha changamoto hiyo ili iweze kutatuliwa kwa maendeleo ya soka la mkoa wa Kilimanjaro na nchi ya Tanzania kwa ujumla.

Mashindano ya Zuberi cup Tournament 2024 vyanatarajiwa kuanza kutimu vumbi Juni mwaka huu ambapo takribani vilabu 32 kutoka ndani na nje ya Manispaa hiyo vitakwenda kushiriki mashindano hayo.






Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.