Akizungumzia suala la upandaji miti ndani ya jeshi hilo, (CGP) Nyamka, amesema jeshi hilo lina kampeni maalum ya upandaji wa miti ikiwa ni kuitikia na kutekeleza maagizo ya wakuu wa nchi, ambayo wamekuwa wakiyasisitiza kuhusiana na utunzaji wa mazingira.
“Malengo ya jeshi la Magereza nchini ni kupanda miti isiyopungua milioni 1.5, ambapo hadi sasa zaidi ya asilimia 50 ya malengo tarajiwa tumekwisha kuyafikia katika zoezi la upandaji wa miti ndani ya jeshi letu”,.
Ameongeza kuwa mazingira yasipotunzwa na kulindwa zipo athari kubwa ambazo kama nchi imekuwa ikizishuhudia hivi karibuni ikiwemo mabadiliko ya tabia nchi na mafuriko, ambayo yote hayo yanachangiwa na shughuli za kibinadamu.
Nao baadhi wa maofisa waliovishwa nishani hiyo akiwemo Mkuu wa Gereza la Loliondo Wilaya ya Ngorongoro Mrakibu George Sosindi na Mkuu wa Gereza la Mkoa wa Tanga Upendo Kazumba, wamemshukuru Rais Samia kwa kuweza kupata fursa ya kuwa miongoni mwa maofisa wachache wa jeshi la magereza kuweza kuvishwa nishani hizo.