Kanisa la Assemblies of God Nazareth Gospel Fire laadhimisha miaka 5; Fungu la Kumi lasisitizwa

Washirika wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God Nazareth Gospel Fire wakiwa katika picha ya pamoja wakati wakiadhimisha miaka mitano tangu kuanza kwa kanisa hilo mnamo mwaka 2019. Kanisa hilo wa sasa linaongozwa na Mchungaji Thomas Massawe. (Picha na. KISENA)


USHIRIKA WA NEEMA, MOSHI 

Kanisa la Assemblies of God Nazareth Gospel Fire limeadhimisha miaka mitano tangu kuanzishwa kwake huku likipanga mikakati ya namna ya kuendelea kuihubiri Injili ya Yesu kwa watu wote.

Akizungumza katika maadhimisho hayo Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Assemblies Of God Thomas Massawe, amewahimiza waumini wa Kanisa hilo kuwa na moyo wa shukrani kwa kumtolea Mwenyezi Mungu shukrani na fungu la kumi katika shida na raha.

“Tangu kanisa letu kuanzishwa tumefikisha miaka mitano, Tumekutana na changamoto nyingi lakini tumemuona Mungu akitushindia,” alisema Mchungaji Massawe  

Hata hivyo Mchungaji Massawe alizitaja changamoto inayowakabili kwa sasa katika kuhubiri Injili ya Yesu Kristo kuwa ni mahali pa kuabudia ambapo kwa sasa wapo katika makazi ya watu.

“Changamoto tuliyonayo, ni eneo la kuabudia liko kwenye makazi ya watu, ambayo tulipewa kwa muda kwa ajili ya kuendesha ibada yetu,” aliongeza Mchungaji Massawe.

Aidha Mchungaji Massawe ametoa wito kwa washirika wake kujitoa katika kufanikisha Injili ya Kristo iweze kusonga mbele kwani wanapokuwa na mahali safi pa kuabudia pia mipango mingine hufanikiwa.

“Washarika kuchangia ununuzi wa kiwanja , kwani eneo tulilopewa tunalilipia kwa kila mwezi. Nimeziona Baraka za Mungu kumtolea Mungu, unapowekeza kwa Mungu huwezi kukuacha kama ulivyo, hata kama unapitia kwenye magumu kiasi gani,” alisisitiza

Kwa upande wake Mzee  wa Kanisa la Assemblies Of God Nazareth Gospel Fire Agripina Thomas Lupembe; alisema wanamengi ya kujivunia katika miaka mitano tangu kuanza kwa kanisa hilo.

“Mungu amekuwa akiponya, huku wengine wamempokea Yesu, hatukutokea sehemu ambayo ilikuwa ni nzuri, bali huduma yetu tulianzia kwenye nyumba iliyokuwa ni Baa na baadae mtu mmoja alitupa eneo lake kwa ajili ya kuabudia kwa muda,” alisema Mzee Lupembe.

Aidha Mtunza Hazina wa kanisa hilo aliwataka washirika kuendelea kumtumaini Mungu siku zote za maisha yao kwani ndiye Muweza wa yote.

“Washirika waendelee kumtegemea Mungu hata katika mapito wanayopitia sasa, Mungu ameanza hapo walipo na watakapozidi kumtumaini Mungu na kumtegemea Mungu atawainua na kuwapelekea ngazi ya juu zaidi,” aliongeza Mtunza Hazina wa Erick Munishi

Kanisa hilo lilianza Mwaka 2019 kwenye eneo ambalo hapo mwanzo ilikuwa ni Baa ya kuuzia pombe. Walikuwa na Washirika Nane, Wanawake 5 na Wanaume 3.

Kwa kipindi cha miaka mitano washirika wameongezeka na kufikia 65, Baraza la Wazee 10, Mashemasi wanane, pia limefanikiwa kuwa na Idara ya wanawake, Vijana na Watoto.







Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.