Wauza Vyakula na Matunda Stendi Kuu Moshi walia na ushuru

MOSHI, STENDI KUU-KILIMANJARO 

Wajasiriamali wa vyakula maarufu Mama Lishe katika Stendi Kuu ya Mabasi mjini Moshi mkoani Kilimanjaro wamepeleka kilio chao kwa Manispaa ya Moshi kuhusu changamoto mbalimbali zinazowakabili wakitaka majibu yenye kuridhisha ikiwamo kiwango cha ushuru wanachotozwa kwa mwezi.

Mama Lishe hao wapatao 150 kati ya wafanyabiashara 467 waliosajiliwa katika stendi hiyo wamekuwa na changamoto lukuki ambazo zimekuwa zikiwakwamisha kutatua changamoto za kifamilia ikiwamo kujipatia malazi, mavazi na chakula kwa ustawi bora.

Wakizungumza na Diwani wa Kata ya Mawenzi Apaikunda Naburi aliyefika katika stendi hiyo na kufanya mkutano wa hadhara wa kujua kero zao ili zipewe utatuzi wa haraka kwa maendeleo yao na taifa kwa ujumla

Aidha Mama Lishe hao wametaka hatua za haraka zichukuliwe dhidi ya watoa huduma wenzao wa vyakula ambao huingia stendi hapo kwa kificho hivyo kukwepa ushuru ambapo wachache ndio wanaobeba mzigo huo.

Katika suala la mama lishe wanaokwepa ushuru, Mwenyekiti wa Akina Mama Lishe  Manispaa ya Moshi Florah Meena, amesema wako baadhi ya akina lishe wamekuwa  wakija alfajiri  na kuzaa vyakula kwenye maeneo  hayo na inapofika majira ya saa moja asubuhi  huondoka pasipo kulipa ushuru.

Aidha katika changamoto ya miundombinu ya maji inayowawezesha kumwaga maji katika stendi hiyo,  Salma Richard, amesema eneo walilotengewa kufanyia biashara ya chakula hakuna sehemu ya kumwaga maji machafu pindi wanapoosha vyombo na wanapo kutwa wakimwaga maji hayo chini hutozwa faini ya Sh elfu 10 na uongozi wa standi hiyo.

Meneja wa Standi Kuu ya Mabasi Moshi Hashimu Kilongola, amesema wako kwa akina mama lishe wamekuwa wakitokea maeneo ya Bomang'ombe, KCMC,  Rau, Machame,  Njoro, na Shirimatunda  na kuondoka asubuhi na hivyo wamekuwa na wakati mgumu wa kuwadhibiti.

Diwani wa  Kata ya Mawenzi Apaikunda Nabur, amesema kikao hicho kiikuwakimelenga kukutana namakundi ya watu wa chini ambao wanafanya biashaara ndani ya standi kuu ya mabasi na akusikiiza kero zao kwani makundi hayo ndiyo yenye changamoto nyingi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Kata ya Mawenzi Mujibu Abeid,  alitumia  fursa hiyo kumuagiza Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi Mwajuma Nasombe,  aliyewakiishwa na Meneja wa Stendi hiyo, kuhakikisha kwamba mama lishe wote wanaofanya biashara ndani ya standi hiyo wanalipa ushuru.




 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.