Aidha wakazi hao katika kipindi cha juma moja za mvua hizo watoto watatu wamefariki dunia kutokana na mafuriko yaliyoharibu miundombinu ya maji, barabara na makazi hatua ambayo imesababisha wakazi hao kuishi katika hali ya taabu na wasiwasi mkubwa.
Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa kijiji cha David Mrema wa Korini Juu amesema mto Mrusunga umefurika maji na kufanya kingo za mto huo kushindwa kuhimili kisha kuyafikia makazi ya watu ambayo yameziacha zaidi ya 300 zikiwa katika wakati mgumu.
Zahanati ya kijiji Kirini Kati, shule za msingi Fukeni, Kwalaa na Mbokomu zimeathiriwa na mafuriko hayo ambayo yameathiri vijiji vitatu vinavyounda kata ya Mbokomu ambavyo ni Korini Juu, Korini Kati na Korini Kusini.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Usambazaji wa Maji na Usafi wa Mazingira (MUWSA) Injinia Innocent Lugodisha amesema kama mamlaka inayoshughulika na usambaji wa huduma ya maji kwa wananchi na usafi wa mazingira inaendeea kufanya tathmini ya uharibifu uliotokana na mafuriko hayo ili kurudisha tena huduma ya maji ambapo hadi sasa kuna shule amabazo watoto hawapati chakula cha mchana kutokana na maji kukosekana kutokana na miundombinu ya maji kuharibika.
"Matengenezo haya sio ya siku mbili wala tatu yatachukua muda ndiyo maana tunaangalia dharura ya kupeleka maji katika kata hii ya Mbokomu; Kata ya Mbokomu imeathirika kwa kiasi kikubwa sana kwa upande wa upatikanaji wa maji safi na salama wako baadhi ya wananchi hawapati kabisa huduma ya maji kutokana na miundombinu hii kusombwa na mafuriko," amesema Injinia Lugodisha.