Watu watano waliofariki kwa mafuriko wilaya ya Moshi mkoani
Kilimanjaro wameagwa leo asubuhi katika viwanja vya Halmashauri ya
Wilaya hiyo na mamia ya waombolezaji.
Tito Chaki (1961-2024),
Joram Kimambo (2011-2024), Freddy Justus (2018-2024), Anjela Chaki
(2012-2024) na Edward Chaki (2010-2024) wa familia moja waliopoteza maisha katika janga hilo.
Walikutwa na umauti
mnamo Aprili 25 mwaka huu, kutokana na Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha
nchini ambazo zimeleta athari kubwa ikiwamo vifo, uharibifu wa
mashamba, nyumba, madaraja na barabara.
Viongozi wa Siasa na dini
wamehudhuria Ibada hiyo na marehemu hao wanatarajiwa kuzikwa katika
kata Mbokomu na Kimochi. wilayani humo.
Bwana Ametoa, Bwana Ametwaa; Jina lake Lihimidiwe.....AMEN