MBUNGE MOSHI MJINI KUANZA ZIARA YA KATA 10 KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI

 

MOSHI-KILIMANJARO.

MBUNGE Jimbo la Moshi Mjini, Alhaji Ibrahim Mohamed Shayo, anatarajia kuanza ziara ya kutembelea kata zote 10 za jimbo hilo kuanzia Novemba 14 hadi Desemba 20, mwaka huu, kwa lengo la kueleza utekelezaji wa miradi ya Serikali ya Awamu ya Sita na kusikiliza kero za wananchi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa CCM Wilaya ya Moshi Mjini, Amos Shimba, kwenda kwa makatibu wa CCM wa kata, ziara hiyo itafanyika kwa awamu ya kwanza kupitia mikutano ya hadhara itakayompa mbunge fursa ya kukutana na wananchi na kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo.

Amesema katika mikutano hiyo, mbunge atatoa taarifa kuhusu miradi mbalimbali ya maendeleo iliyotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita katika jimbo hilo, huku akisikiliza changamoto na kero zinazowakabili wananchi ili kuzitafutia ufumbuzi.

Amesema ziara hiyo itaanza Novemba 14, mwaka huu, katika Kata ya Rau, ambapo mkutano wa hadhara utafanyika eneo la Rau Madukani, kabla ya kuendelea Novemba 15 katika Kata ya Shirimatunda.

Kwa mujibu wa ratiba hiyo, Novemba 22 atatembelea Kata ya Soweto, huku Novemba 28 akitarajiwa kufanya mkutano wa hadhara katika Kata ya Bomambuzi.

Aidha, ratiba inaonesha kuwa Desemba 5 atakuwa katika Kata ya Pasua, Desemba 6 Majengo, Desemba 12 Korongoni na Desemba 13 Njoro.

Kata nyingine zitakazotembelewa ni Kaloleni Desemba 19 na Kiborloni Desemba 20, mwaka huu, ikiwa ni sehemu ya ziara hiyo inayolenga kuimarisha mawasiliano kati ya mbunge na wananchi pamoja na kupata maoni yao kuhusu utekelezaji wa shughuli za maendeleo jimboni humo.





Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.