TCB YALENGA KUPANDISHA UNYWAJI KAHAWA NCHINI HADI ASILIMIA 15

MOSHI-KILIMANJARO 

BODI ya Kahawa Tanzania (TCB) imelenga kuongeza kiwango cha unywaji wa kahawa nchini kutoka asilimia saba ya sasa hadi asilimia 15, ili kupanua soko la ndani na kuongeza matumizi ya kahawa inayozalishwa na wakulima wa Tanzania.

Mkurugenzi Mkuu wa TCB, Primus Kimaryo, alisema hayo wakati wa Tamasha la Saba la Kahawa lililofanyika mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro.

Alibainisha kuwa tangu tamasha hilo lilipoanzishwa mwaka 2019, kiwango cha unywaji wa kahawa nchini kimeongezeka kutoka chini ya asilimia tatu hadi kufikia asilimia saba.

Kimaryo alisema lengo la bodi hiyo ni kuendelea kuhamasisha Watanzania kunywa kahawa inayozalishwa nchini, hatua itakayosaidia kukuza soko la ndani na kuongeza fursa za kibiashara kwa wakulima na wadau wengine katika mnyororo wa thamani wa zao hilo.






Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.