NUSU FAINALI ZUBERI CUP KUANZA AGOSTI 16



MOSHI-KILIMANJARO.

NUSU fainali ya mashindano ya Zuberi Cup inatarajiwa kuanza Agosti 16, 2026, katika Uwanja wa Railway Njoro, Moshi, huku La Familia FC ikitarajiwa kukutana na Kili Warriors FC katika mchezo wa kwanza wa hatua hiyo.

Akizungumza kuhusu ratiba hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Zuberi Cup, Japhet Mpande, amesema nusu fainali ya kwanza itachezwa Agosti 16 katika Uwanja wa Railway Njoro, ambapo timu hizo mbili zitachuana kusaka nafasi ya kufuzu hatua ya fainali.

Mpande amesema mchezo mwingine wa nusu fainali utawakutanisha Kili Plantation FC na mshindi kati ya Fire FC na Hai United, ambazo zinatarajiwa kukutana kesho katika mchezo wa robo fainali utakaochezwa Uwanja wa Railway Njoro.

Amesema mshindi wa mchezo huo ataungana na Kili Plantation FC katika hatua ya nusu fainali, huku mchezo huo ukitarajiwa kuchezwa Agosti 22, 2026, kabla ya fainali ya mashindano hayo kuchezwa Agosti 23, mwaka huu.

Kwa upande wa mashabiki wa soka, hatua hiyo inatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na timu zilizofuzu kuendelea kusaka nafasi ya kutwaa ubingwa wa Zuberi Cup, huku kila timu ikihitaji kutumia nafasi hiyo kuonyesha uwezo na kupigania taji hilo.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.