KILI WONDERS FC YATINGA FAINALI BAADA YA KUICHAPA LA FAMILIA FC 3-1


MOSHI-KILIMANJARO.

TIMU ya Kili Wonders FC imefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya Mashindano ya Zuberi Cup baada ya kuichapa La Familia FC mabao 3-1 katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza uliochezwa Uwanja wa Railway Njoro, Moshi.

Kili Wonders ilianza kwa kasi na dakika ya 30 ya kipindi cha kwanza, Idd Mussa aliifungia timu yake bao la kwanza, kabla ya Alexander Vicent kuongeza bao la pili dakika ya 38 na kuifanya Kili Wonders kwenda mapumziko ikiwa mbele kwa mabao 2-0.

Kipindi cha pili, Kili Wonders iliendelea kutawala mchezo na dakika ya 51, Alexander Vicent alifunga bao lake la pili katika mchezo huo na la tatu kwa timu yake, na kuifanya La Familia FC kuwa katika wakati mgumu wa kurejea mchezoni.

La Familia FC ilipata bao la kufutia machozi dakika ya 83 kupitia kwa Hamisi Tambwe, lakini halikutosha kubadili matokeo ya mchezo huo.

Mpaka filimbi ya mwisho, Kili Wonders iliibuka na ushindi wa mabao 3-1 na hivyo kutinga fainali ya mashindano hayo.





















Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.