MOSHI-KILIMANJARO.
MBUNGE wa Jimbo la Moshi Vijijini Morris Makoi, amenunua mitambo ya ujenzi na ukarabati wa barabara kwa lengo la kuboresha miundombinu na kuhakikisha barabara za vijijini zinapitika wakati wote, hatua inayotekeleza ahadi aliyotoa kwa wananchi wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
Mitambo hiyo ambayo inatarajiwa kuzinduliwa Julai 14, mwaka huu, inatarajiwa kutumika katika shughuli za ujenzi, ufunguaji na ukarabati wa barabara katika kata 16 za Jimbo la Moshi Vijijini ikiwa ni sehemu ya juhudi za kurahisisha usafiri na usafirishaji na huduma nyingine muhimu kwa wananchi.
Katibu wa Mbunge wa Jimbo laMoshiVijijiniAlly Badi, ameyasema hayo leo Jumapili Julai 12,2026 wqkqti akizungumza na KISENAUPDATE.BLOGSPOT.COM, ambapo amesema uzinduzi rasmi wa mitambo hiyo utafanyika Julai 14, mwaka huu, katika Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Moshi zilizopo Sango, Kata ya Kimochi.
Badi; amesema upatikanaji wa mitambo hiyo utasaidia kupunguza utegemezi wa vifaa kutoka maeneo mengine na kuongeza kasi ya matengenezo ya barabara zinazoharibika hasa wakati wa mvua.
"Kwa muda mrefu wananchi wa Jimbo la Moshi Vijijini, wamekuwa wakilalamikia ubovu wa miundombinu ya barabara, hali inayosababisha uharibifu wa vyombo vya usafiri, kupanda kwa gharama za usafiri na kuchelewesha shughuli za kiuchumi na kijamii.
Kwa upande wake Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Wilaya Moshi Vijijini na Mjumbe wa Baraza la Wazazai mkoa wa Kilimanjaro Wakiki Emanuel Mlaki, amewapongeza wabunge wa majimbo hayo huku akisema kuwa wanatekelwza Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi CCM.
Aidha Mlaki alisema mitambo hiyo itasaidia kuboresha barabara, madaraja na kurahisisha shughuli za kiuchumi.
" Uwekezaji huo utasaidia kufungua maeneo yaliyokuwa magumu kufikika, kuimarisha huduma za kijamii na kuchochea ukuaji wa uchumi kupitia usafirishaji rahisi wa mazao na bidhaa nyingine."alisema Adv Mlaki.





