MALEZI BORA YATAJWA KUWA MSINGI WA MAFANIKIO YA WATOTO

MOSHI-KILIMANJA.


DIWANI wa Kata ya Kiusa, Khalid Shekoloa, amesema malezi bora kwa watoto ndiyo msingi muhimu wa kujenga jamii yenye maadili, uwajibikaji na mafanikio ya baadaye.

Shekoloa alisema Wazazi na Walezi wanapaswa kutumia muda wa kutosha kuwa karibu na watoto wao ili kuwajengea maadili mema, nidhamu na kuwasaidia kutambua umuhimu wa elimu katika maisha yao ya baadaye.

Alieleza kuwa changamoto nyingi zinazojitokeza katika jamii, ikiwemo utoro wa shule, matumizi ya dawa za kulevya na ukosefu wa maadili, zinaweza kupungua iwapo wazazi watachukua jukumu lao kikamilifu katika malezi ya watoto.

Diwani huyo alitoa rai kwa jamii kuendelea kushirikiana katika kuwalea watoto kwenye misingi ya heshima, upendo na uwajibikaji ili kuwaandaa kuwa viongozi na wananchi wema wa taifa hapo baadaye.





Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.