PRISCUS TARIMO; WASHUKURU UWT MOSHI MJINI KWA USHIRIKIANO WAO WALIOMPA

MOSHI-KILIMANJARO.

KATIKA  hotuba yake, Priscus Tarimo, aliwashukuru wanachama wa UWT Wilaya ya Moshi Mjini kwa mchango wao katika mafanikio yake ya kisiasa na utekelezaji wa ilani ya CCM wakati wa kipindi chake cha miaka mitano bungeni.

“Ninaamini ushindi wangu ndani ya chama usingewezekana bila ninyi UWT. Nawashukuru sana kwa ushirikiano wenu mkubwa,” alisema.

Aliongeza kuwa mafanikio yaliyopatikana katika jimbo la Moshi Mjini, yakiwemo utekelezaji wa miradi ya maendeleo, yalitokana na mshikamano na sapoti ya wanawake hao.

AIZUNGUMZIA MIRADI YA MAENDELEO MOSHI;

Tarimo alitaja baadhi ya miradi aliyoisimamia akiwa mbunge, ikiwemo kurejea kwa wakandarasi katika mradi wa ujenzi wa stendi mpya ya mabasi ya Ngangamfumuni, ambao kwa sasa unaendelea.

Pia alieleza kuwa alipigania kurejeshwa kwa mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, baada ya kusitishwa kwa muda.

“Nilipigania kwa nguvu zote bungeni kuhakikisha mikopo hiyo inarejeshwa, na hatimaye serikali ilikubali kuirejesha,” alisema.

Aidha, aligusia juhudi za kuendeleza miundombinu ya usafiri wa anga katika eneo la Moshi, akisema kuwa alishiriki kushawishi serikali kutenga fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi na uboreshaji wa uwanja wa ndege wa Moshi.

Akizungumzia mustakabali wa Moshi, Tarimo alisema ana imani kuwa ndoto ya Moshi kuwa Jiji bado ina nafasi ya kutimia chini ya uongozi wa wabunge na viongozi waliopo sasa.

Alimaliza kwa kusisitiza umuhimu wa Umoja, Mshikamano na kuendelea kusimamia haki za Wanawake katika siasa na maendeleo ya jamii kwa ujumla.




Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.