WATU WATANO WAFARIKI KWA AJALI YA HELIKOPTA YA UOKOAJI KINAPA

MOSHI-KILIMANJARO.

WATU watano wamefariki dunia katika ajali ya helikopta ya Kampuni ya KiliMedair iliyokuwa ikifanya shughuli za uokoaji katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA).

Mhifadhi Mkuu wa Huduma za Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Kamishna wa Uhifadhi Musa Kuji, ameyasema hayo Desemba 25,2025 mjini Moshi, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na ajali hiyo.

Amesema ajali hiyo ilitokea Jumatano majira ya saa 11:30 jioni katika eneo la Kambi ya Barafu, ndani ya hifadhi hiyo, Wilaya ya Moshi mkoani humo.

Kwa mujibu wa Kamishna Kuji, amesema ajali hiyo ilitokea katika eneo la Kambi ya Barafu lenye urefu wa mita 4,673 kutoka usawa wa bahari, ambalo ni sehemu ya Mlima Kilimanjaro.

Ambapo ajali hiyo ilihusisha helikopta ya uokoaji ya kampuni ya KiliMedair na kusababisha vifo vya watu watano akiwemo mwanamke mmoja.

Aidha Kamishna Kuji ameongeza kuwa mawasiliano kati ya mamlaka za Tanzania na Ubalozi wa Jamhuri ya Czech nchini tayari yameanza ili kukamilisha taratibu za utambuzi wa miili ya raia hao wa kigeni na hatua nyingine zinazohusiana na msiba huo.





Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.